Ketoka
JF-Expert Member
- Sep 23, 2015
- 1,117
- 1,966
Huu Uzi maalumu kwa ajili ya watumishi wa umma wenye salary slip na check no ambao kwa miaka 5 tumedhulumiwa haki yetu
Serikali ya ccm haina muda na watumishi, increments kwa watumishi zimetupiliwa mbali
Watumishi tumejikuta tunafanya kazi nyingi na ngumu kisa serikali haijiri,hili linawakumba walimu na kada ya afya
Nyongeza ya mishahara ndo hivyo tena, wastaafu kupata mafao yao mpaka mungu ashuke.
Madaraja kupanda ilikuwa miaka 3 ila sasa imepelekwa hadi miaka 4, ambapo sisi watumishi tunajua daraja ndo mshahara,sasa kama madaraja hayapandi mbona mishahara yetu ina hali ngumu,na pamoja kuongeza miaka ya kupanda daraja, ukifika hata hawapandishi tena wale ambao wangepanda mwaka huu ndo hivyo tena.
Ukienda masomoni tena inakuwa dhambi kubwa ya kujiendeleza,ccm hawataki watumishi wajiendeleze ndo maana waliokuwa masomoni hawakupandishwa madaraja
Vyama vya wafanyakazi hawana sauti, hawafurukuti.
Pamoja na matatizo mengi tuliyonayo bado serikali imeshindwa kutuweka mazingira mazuri kwa wafanyakazi
Tukiwa kama wapiga kura na wengine watakuwa wasimamizi na tukiwa na hazina ya wanaotutegemea huko nyuma kura zetu zinatosha kuonyesha serikali hii kuwa hatuitaki.
Kwa wale ambao watasimamia uchaguzi kwa niaba ya Tume lazima tuje kufanya yetu.
Watumishi wa umma njoo tuiondoe serikali hii madarakani.