Watumishi wa umma wachangishwa ujenzi wa maabara

HOBBIES

Senior Member
Joined
Dec 29, 2011
Posts
145
Reaction score
17
30th September 2014



Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba


Serikali imebuni utaratibu wa kuchangisha fedha za ujenzi wa maabara kwa kuwachangisha walimu na watumishi wengine wa umma.

Zoezi hilo linatekelezwa na wakurugenzi watendaji wa halmashauri nchini, ambao baadhi wameandika barua kwa waratibu elimu wa kata kutekeleza uchangishaji huo na kuwasilisha fedha hizo kwenye halmashauri.

Kwa mujibu wa barua ya Septemba 15, mwaka huu, kutoka moja ya halmashauri nchini (jina limehifadhiwa) kwenda kwa waratibu wa elimu wa kata, ikiwa na kichwa cha habari cha `Michango ya maendeleo kuchangia ujenzi wa maabara', imewataka waratibu hao kukusanya fedha hizo kutoka kwa walimu.

Aidha, barua hiyo ambayo NIPASHE imeiona nakala yake, imeeleza kuwa kulingana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya ukamilishwaji wa maabara katika shule zote za sekondari nchini, uongozi wa halmashauri umeridhia uchangiaji huo.

“Kwa barua hii, naagiza uchangiaji wa ujenzi wa maabara kutokana na maamuzi ya wilaya,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.

Barua hiyo ilitaja viwango vya uchangiaji kuwa ni Sh. 60,000 (waratibu elimu kata), Sh. 60,000 (walimu ngazi ya mshahara TGTS F-G), Sh. 30,000 (ngazi ya mshahara TGTS D-E) na Sh. 20,000 ( TGTS B-C).

Aidha, barua hiyo ilieleza kuwa michango hiyo itatolewa kwa awamu mbili Septemba na Oktoba, mwaka huu.

Barua hiyo pia imeagiza walimu wakuu kusimamia michango hiyo kwa shule zao na kufikisha fedha hizo halmashauri.

Katika Wilaya ya Same, baadhi ya wakuu wa shule walisema wamepata maelekezo ya wazazi wenye watoto wa kidato cha kwanza kuchangia Sh. 30,000 na kidato cha pili hadi sita kuchangia Sh. 20,000, ambazo zinapaswa kuwasilishwa kwa wakuu wa shule, ambao watazipeleka halmashauri.

Baadhi ya wauguzi waliozungumza na NIPASHE kwa njia ya simu kutoka mkoani Manyara, walithibitisha kupewa barua zinazowataka kuchanga fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa maabara nchi nzima.

“Tumeuliza juu ya utaratibu huu, wamesema ndiyo utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)…mchango huu unafanywa kama wa lazima kwa kuwa msimamiaji ni bosi wa walimu,” alisema mmoja wa wauguzi.

Aidha, baadhi ya walimu wamelalamikia utaratibu huo na kueleza kuwa kwa kuwatumia walimu umeonekana kuwa wa lazima, huku walimu wakiwa na mishahara duni, madai serikalini na kudhulumiwa stahili zao mbalimbali.

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, alithibitisha kupokea malalamiko ya walimu kwenye wilaya tofauti nchini.

“Nilipokea malalamiko yakielezea barua hiyo inayowataka kuchangia. Tumewaagiza viongozi wa CWT kushughulikia ili iwe kwa hiari na siyo kukatwa kwenye mishahara,” alisema Mukoba.

Alisema iwapo fedha hizo zitakatwa moja kwa moja kwenye mishahara ya walimu haitakuwa sahihi.Mukoba alisema makato ya kisheria yamewekwa wazi, ambayo ni mfuko wa hifadhi ya jamii na kodi.

Hivyo, akasema inapojitokeza michango mingine, maamuzi yanapaswa kufanywa na walimu wenyewe na siyo kutoa maelekezo kutoka juu kwenda chini.“Mwalimu ndiye atoe idhini ya mshahara wake kukatwa.

Siyo vibaya maabara kujengwa. Lakini tatizo mchangishaji ni nani? Kuwatumia barua kutoka ngazi ya juu, ni kama kuwalazimisha bila kuongea nao,” alisema Mukoba.

Alisema ni vyema maamuzi yakaanzia chini kwa walimu wenyewe kuliko inavyofanyika sasa, kuanzia juu, ikiwa ni pamoja na kuwa na utaratibu wa wazi ambao haugubikwi na kiini macho.

“Lazima ijulikane mkusanyaji ni nani, atakusanya kiasi gani na atapeleka kiasi gani kwenye ujenzi huo. Tunahofia matumizi mabaya ya fedha,” alisema Mukoba.

NIPASHE ilimtafuta Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema hana taarifa kuhusiana na suala hilo na kuelekeza aulizwe Katibu Mkuu.

NIPASHE
 
Agizo la mh jk kwa wa kuu wa wilaya kuwa wakamiliashe ujenzi wa mabara mashuleni na baadhi ya wilaya kutoa matamko kuwa watakata shilingi elfu 40 kwa kila mwalimu toka katika mshahara wa mwalimu

miye naona sasa serikali kupitia wakuu wa wilaya wake inataka vuka mipaka kuwachezea walimu
na kama ilikuwa inawatafuta sasa imewapata

ukweli walmu damu changa iliyotoka vyuoni hawata kubali huu upuuzi
 
Wanataka kutupanda vichwani sasa. Nadhani wamechoka na sisi hawa washenzi kabisaaaa. Ki ukweli nikikatwa hiyo hela nitakuwa wa kwanza kuchukuliwa hatua kwa kugoma kufanya kazi na nitaacha kabisa fani.
 
Dah hizi ndo effects za serkali dhaifu, mwalimu mshahara ni sh. Ngapi hadi umkate elfu40? Jamani hizi dhambi hawa mafisadi wanaolipwa laki 3 kwa siku watakuja kwenda kuzitubia wapi?
 
Dah hizi ndo effects za serkali dhaifu, mwalimu mshahara ni sh. Ngapi hadi umkate elfu40? Jamani hizi dhambi hawa mafisadi wanaolipwa laki 3 kwa siku watakuja kwenda kuzitubia wapi?

Dr Fastjet na wakurugenzi wake nahisi wamevimbiwa hadi wanashindwa kufikiri!
Alafu hapo kuna walimu bado wanashabkia ccm.
 
Dr Fastjet na wakurugenzi wake nahisi wamevimbiwa hadi wanashindwa kufikiri!
Alafu hapo kuna walimu bado wanashabkia ccm.



Mkuu Rigo ujenzi Wa maabara ni kwa faida yetu sote si CCM peke yake
 
Mkuu Rigo ujenzi Wa maabara ni kwa faida yetu sote si CCM peke yake
sasa wewe kama unaona ni kwa faida ya watu wote basi kila mtumishi wa umma achangishwe hiyo hela au kama vip kila mtumishi achangie ujenzi wa taasisi anayofanyia kazi sio suala la kuonea baadhi ya watumishi tu yaani kila kitu waalimu na wauguzi jkt wao na michango pia yaani haya majinga ya ccm nayachukia yaani nimgekuwa na uwezo ningeomba yafe yote ili tuanze kuijenga upya tanzania yetu!!!!
 
Naisubir hyo barua ije huk kwet kigoma ila namshukuru mungu hapa shulen kwangu kuna maabara na vifaa vya kutosha.
 
mtumishi anakatwa kodi na kodi ipo kwa ajili ya maendeleo so eachukue kodi ya mtumushi ya mwezi mmoja waipeleke kwenye ujenzi si jukata take home ya mtu yani kodi wakate and then na take home warambe hapana hii sio vizuri kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…