Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Umeshakatwa mshaara jomba tulia,utawala huu inabidi ufuate taratibu na uacha tamaa.
 
2024 Hadi 2025 tutaelewana tu .na tutaongea lugha moja

Mmesitishiwa mshahara wa mwezi 1 tu mnapiga piga kelele kelele,sasa hivyo vitisho vya kusubiri 2024-25 ni sawa na kutishia kujamba wakati unaharisha.

Mapinduzi daimaaaa,kidumu chama.
 
Walizoea kwamba ukigombea kupitia CCM hutoguswa na mkono wa sheria huku wakitegemea kupata teuzi mbalimbali. Nyoosha nchi baba watu wajifunze kufuata sheria na sio mazoea.
Nawasikitikia lakini wajifunze kuacha tamaa.na ajabu wote hao utakuta wametia nia ccm.
 
Weka Sheria hiyo hapa Kama unachokiongea unakifahamu au wewe Ni wale walio unga unga madarasa na vyuo.
Likizo bila malipo inachukuliwa wakati wa mchakato wa kura za maoni na ukishateuliwa kupeperusha bendera ya chama chochote unatakiwa uache kazi hata kama ktk uchaguzi utashindwa ndo bye bye, watumishi wa umma mnapaswa kuyajua haya kwa sababu wasimamizi wenu wanazo nyaraka zote.
 
Weka Sheria hiyo hapa Kama unachokiongea unakifahamu au wewe Ni wale walio unga unga madarasa na vyuo.
Huu ni waraka wa mkuu wa utumishi wa umma sio sheria. Waraka huu hata JPM ameukuta, kinachofanyika ni kutekeleza tu. Kama ni mtumishi nenda kamuone mkuu wako wa Idara ya utawala au Afisa utumishi utapata huo waraka. Mimi ninao lkn kwa vile maadili yangu kama mtumishi nayaelewa siwezi kuweka hapa huo waraka maana haukuwa kwa matumizi ya watu wote.
 
Sheria hii haisemi au haiongei habari ya kutia nia.insongelea habari ya kugombea nafasi za kisiasa.tambua kutia Nia ni kuchukua fomu Tena unauziwa na chama tawala. Leave inayodemewa watia Nia hawajafika hatua ya kuomba leave without pay. Kwa taarifa yako ukitoka Nia na kuteuliwa kugombea chama husika hakitakuruhusu kujaza fomu ya time ya kugombea bila kuwakabidhi barua ya leave without pay.Kifungu hiki ulicho tuma sio.
 
Mwaka 2000,2005,2010 na 2015 walichukua mishahara ya waliotia Nia? Kule Jimbo la biharamulo na chato wakati huo mgombea alikuwa Nani na alipotia Nia akiwa walimu sengerema sekondari alifanyiwa hayo?
Using'ang'anie ujinga wewe. Kama watu hawakufungwa kwa kubaka mwaka 1960 kwasababu sheria haikutaka wafungwe unataka na leo wasifungwe? We tumikia maelekezo halali ya serikali na kama hukuomba ruhusa unastahili hata kusimamishwa kazi maana unajifanya una kihelehele sana
 
Jibu swali,mbona unaleta ngonjera JF
 
Mwaka 2000,2005,2010 na 2015 walichukua mishahara ya waliotia Nia? Kule Jimbo la biharamulo na chato wakati huo mgombea alikuwa Nani na alipotia Nia akiwa walimu sengerema sekondari alifanyiwa hayo?
Usipokuwa makini na kazi inaenda kuota mbawa,

Ukisikia matumizi ya mali ya umma kwa manufaa binafsi ndiyo hayo, umeenda kwenye kazi zako binafsi na hujafanya kazi ya umma mshahara unalipwa kwa lipi.....!

Uwepo wa sheria na usimamizi wa sheria ni mambo mawili, sheria ilikuwepo ila wasimamizi hawakuamua kuisimamia utekelezwaji wake so utetezi wako ni mfu.

Subiri kesi ya kushiriki kwenye siasa bila idhini ya mwajiri huku ukiwa mtumishi wa umma pamoja na kudanganya kwamba una attend family matters kumbe siyo.
 
Sheria ya kipumbavu kwasababu imekugusa wewe?? Rais na mawaziri nafasi zao ni za kuchaguliwa, hivyo ni lazima watie nia, wewe mtumishi wa umma huwa unachaguliwa? Tusipindue taratibu kwasababu zimetubana bali tujifunze kufuata taratibu. Kitendo tu cha kutia nia maana yake wewe una maslahi na chama fulani, unaweza kutumia Mamlaka yako vibaya kama tusipokutoa kwenye utumishi temporarily.
 
This is true, naifahamu hii vizuri sana na ndivyo ilivyo
 
Poleni sana wadau wenzangu kwa kadhia iliyotukuta pamoja. Tunaamini tulitumia haki yetu ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa. Tatizo ni kuwa kwenye taasisi za serikali. Nawapa pongezi wenzetu wa taasisi na mashirika yasiyo ya serikali kwa kutumia haki yao bila bughudha. Tuzidi kushikamana kipindi hiki cha majonzi mara tatu. Kwa kuambulia kura 0,1, na 3, kwa kufiwa na kipenzi chetu Mkapa, na kwa kuanza maisha mapya ya kuomba omba nauli na kukopa kwenye maduka ya mpemba na mangi. Tusijali, Mungu atatufuta machozi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…