Watumishi wa umma wapewe 'performance contract'?

Kikojozi

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2009
Posts
331
Reaction score
2
Heshima kwenu wanajamii.

Katika jitihada za kuongeza ufanisi sekta ya utumishi wa umma, nilikua napendekeza watumishi wote wa umma wapewe mikataba ya ajira inayomwezesha muajiri na wateja/wadau wote wa mashirika ya umma na ofisi za serikali kutathmini utendaji wao.

Hii ni tofauti na utaratibu wa sasa ambapo mtu anaajiriwa serikalini kwa 'permanent and pensionable terms'. Wakisha kamata ajira wenyewe wanasema mpaka kufukuzwa yaani uwe "umeboronga sana". Kwahiyo hata kama mtu hafanyi kazi kwa uadilifu anaendelea tu kuwepo kwenye ajira huku vijana wengi wanaomaliza vyuoni na wana uwezo wanakosa kazi. System ya sasa inavumilia mno uzembe na rushwa.

Ajira za serikali na mashirika ya umma iwe ya mikataba isiyozidi miaka mitano na ku-renew itategemea kama utendaji wa mtu unaridhisha.

Wadau mnalionaje suala la 'performance contracts' kwa watumishi wa umma?
 
Hii ni safi sema utekeleza mgumu! hivi mfano waalimu wa sayansi wako wachache, na unawapa contract ya 5 years na unampeleka kule Ruangwa! shule ina waalimu watatu!

Je wanafunzi wasipofaulu je..huyo mwalimu contract iishe? Shule ibaki kabisa bila kuwa na waalimu?

Taabu ya Tz mazingira ya kazi ni magumu sana na yanatofautiana kwa aina ya kazi na sehemu mtu anapofanyia kazi!
 
..we should start with the President, VP, Prime Ministers, Ministers,and MPs.

..if those knew that their stay in office depends on some kind of 'performance contract', then they sure will shake things up and demand productivity and accountability from civil servants.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…