DOKEZO Watumishi wa Umma zaidi ya 80% hawajapandishwa madaraja ndani ya mwaka wa fedha 2023/2024 unaoisha. Hii ni dhulma kubwa

DOKEZO Watumishi wa Umma zaidi ya 80% hawajapandishwa madaraja ndani ya mwaka wa fedha 2023/2024 unaoisha. Hii ni dhulma kubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
WIZARA YA UTUMISHI WA UMMA INVYOWADHARAU WATUMISHI WA UMMA

1. Wizara ya Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa UMMA nna Utawala Bora ilitoa waraka au tuseme kibali cha upandishaji madaraja kwa watumishi wa Tanzania tarehe 28 Mei 2024

2. Wenye kichwa cha habari UPANDISHAJI WA VYEO [PROMOTION] NA
UBADILISHAJI WA KADA /MUUNDO WATUMISHI [RECATEGORIZATION] KWA MWAKA 2023/2024

3. Muongozo huo uliwataka kupandisha watumishi wote wa Umma waliotengewa bajeti [Ikama] 2023/2024

4. Muongozo huo uliwataka waajiri kuhakikisha mpaka kufika June 3 ,2024 zoezi ilo linakamilika na wizara nayo ingekamilisha kwenye mfumo wa kiutumishi na mishahara [HCMIS] June 6, 2024 maana yake ndani ya siku 29 kila kitu kikamilike na watu wapate mishahara, ukitoa siku za mapumziko maana yake ndani ya siku 19 tu kila kitu kingekamilika

5. Hapa ndio dharau za wizara ya Utumishi inapoanza kudharau watumishi wa Umma, wanajua kabisa siku hizo 30 au wakipewa siku 60 hawataweza kupandisha watumishi wote wa UMMA TANZANIA ambao wanakadiliwa zaidi ya Elfu 52 ni kuwacheza Shere tu watumishi wa UMMA

6. Baada ya Watumishi wa UMMA kupokea mishahara yao watumishi waliotegemea kupanda madaraja zaidi ya 80 Tanzania 🇹🇿 hawajapanda Madaraja, kisingizio ni Aprova ambao wapo wizara ya UTUMISHI kimsingi inaweza kuwa kweli au si kweli .

7. Serikali inajua ilikua inategemea kuwapandisha watumishi wa Umma mwezi June 2024 kwanini zoezi la kuingiza taarifa za kiutumishi zisianze mapema mwezi January ili ikifika mwezi June watumishi wapandishwe mishahara

8. Serikali imekuwa ikiwadharau watumishi wa Umma, bajeti inapitishwa Julai 2023 na utekelezaji wa Bajeti unaanza mara moja kwa kila kitu, lakini kwenye promosheni ya watumishi wa Umma inaenda mwaka unaofuata wa 2024 hizo zote ni dharau kwa watumishi wa Umma

9. Serikali inapokuwa na jambo linalohitaji utekelezaji kwa watumishi mikwara ni mingi sana kwa watumishi umeletwa mfumo wa ESS kwa watumishi Umma, watumishi wengi walioshindwa kujiunga kwa wakati wamekosa mishahara huu sasa mwezi wa tatu na wengine ni wanne

Watumishi wa Umma, wameamua kupaza sauti zetu, tunaomba kilio cha wa watumishi wa Umma kifike IKULU kwa Mama, wamechoka kudharauliwa mwezi huu kuna watumishi wa Umma wamepata Promosheni kuna wengine hawajapata je kunawezaje kuwa na usawa kwa watumishi hao wa Umma ukizingatia wote walitakiwa kupanda ndani ya mwaka wa fedha 2023/2024 ambao unaisha ndani ya Mwezi huu .

Maana yake watumishi wengine wa Umma wanaenda kupanda mwaka mwaka 2024/2025 kuminya haki kwa watumishi wa Umma, tunaomba Jamii Forums muwasiliane na Katibu Mkuu Utumishi wa Umma na Waziri wake watoke mbele za Umma wawaeleze watumishi wa Tanzania kwanini watumishi wa Umma karibia 80% hawajapandishwa kwa wakati
 
yaan aliyeandaa huu waraka Kuna watu amewasahau kabisa,serikali ilisema italinganisha vyeo Kwa watumishi wote wa umma lakin Bado jambo hili halijafanyika kabisa
 
Hii
yaan aliyeandaa huu waraka Kuna watu amewasahau kabisa,serikali ilisema italinganisha vyeo Kwa watumishi wote wa umma lakin Bado jambo hili halijafanyika kabisa
Nchi ni noma. Ngoja tuone njia ya muongo ni fupi sana
 
WANAMTUMA MSONDE KU SPIN HILO SWALA KWA VIKAO VYA KISHENZI KWA WALIMU NCHINI!!

HALAFU WANATUOMBA KURA TUMPITISHE SAMIAH KWA KISHINDO!!

WATAMPITISHA WANAJESHI NA POLICE HAO NDIO KAZI YAO NCHINI!!
 
Waliokaa miaka 5 bila kupandishwa daraja Wala kuboreshewa maslahi yeyote lakini mwaka huu tuu mmja imekuwa nongwa na lawama kama zote.

Mumesahau haya? 👇👇

View: https://twitter.com/mamanafanikisha/status/1806947199550398886?t=YgjgUEUCrILnny2q3l1agA&s=19

Mnapopenda kusifiwa kupitiliza, muwe pia mnakubali kukosolewa. Hata hiyo awamu unayoiongelea, watumishi wa umma walipaza sauti zao humu jukwaani juu ya huo uonevu wa kuminya haki za watumishi wa umma kwa sababu za kipuuzi za kununua ndege, na bla bla nyingine.

Mtoa mada ana hoja. Hivyo anatakiwa asikilizwe na mamlaka husika zichukue hatua. Ubabaishaji na uonevu kwa watumishi wa umma, haukubaliki.
 
WANAMTUMA MSONDE KU SPIN HILO SWALA KWA VIKAO VYA KISHENZI KWA WALIMU NCHINI!!

HALAFU WANATUOMBA KURA TUMPITISHE SAMIAH KWA KISHINDO!!

WATAMPITISHA WANAJESHI NA POLICE HAO NDIO KAZI YAO NCHINI!!
Msonde nilikuwa namheshimu sana. Utendaji wake na mahusiano yake na walimu kwenye kazi maalumu alipokuwa Baraza la Mitihani yalikuwa mazuri. Sijui amekuwaje, maana alizunguka nchi nzima kuwaaminisha walimu kuwa watapanda madaraja hasa wale waliopunjwa.
 
Msonde nilikuwa namheshimu sana. Utendaji wake na mahusiano yake na walimu kwenye kazi maalumu alipokuwa Baraza la Mitihani yalikuwa mazuri. Sijui amekuwaje, maana alizunguka nchi nzima kuwaaminisha walimu kuwa watapanda madaraja hasa wale waliopunjwa
 
Mawaziri wenye dhamana wote wapo kimya,Kuna kipindi nafikiri mwez wa tatu Maafsa utumishi waliitwa dodoma ili kupitia watumishi mmoja baada ya mwingine lengo ikiwa ni kufanya harmonization(msawazisho ,),wa vyeo lakin Hilo jambo limewekwa kibindoni na wenye changamoto hii ni wengi sasa wasiposhughulikiwa changamoto Yao si moyo wa kufanya Kaz utapungua,?,mbaya Zaid Dr Msonde ,Mchengerwa ,Ridhiwani hawaongelei tena hili jambo
 
Tulia..
Madaraja yanaendelea badilishwa. Ingia PEPMIS ...
 
Dah mimi niliingia jana kwenye pempsi, kisha nikalog out then nikalog in na ku click profile na kukuta mabadiliko kwenye designation , huenda july hii ni 💰 💰💰💰💰
 
Back
Top Bottom