Watumishi wa Halmashauri ya Ushetu, Wilaya ya Kahama, tumekuwa tukikumbana na changamoto ya kubadilishiwa vituo vya kazi bila kufuata taratibu stahiki. Aidha, watumishi wanaohamishwa hawapewi stahiki zao za uhamisho kama walivyoomba kupitia barua zao zilizowasilishwa katika Ofisi ya Mkurugenzi.
Badala ya kulipwa stahiki zinazostahili kwa mujibu wa kanuni na taratibu za utumishi wa umma, baadhi ya watumishi wanapewa kiasi cha shilingi 500,000 tu kama malipo ya jumla, bila maelezo ya kina kuhusu fedha hizo na msingi wake wa kisheria.
Tunaomba suala hili lipaziwe sauti ili watumishi wapate haki zao za msingi. Ikiwa Halmashauri haina fedha za kugharamia uhamisho wa watumishi, tunaomba viongozi husika, ikiwemo CHMT, Katibu wa Afya na DMO, wasitumie mamlaka au nafasi zao kuwakandamiza watumishi wa afya kwa kuwahamisha bila kuwalipa stahiki zao halali.
Mimi ni mtumishi kada ya afya halmashauri ya ushetu imekuwa ikibadilishia watumishi vituo bila ya kuwalipa sitahiki zao za uhamisho hata bila taarifa zozote kisa tu msimamizi WA kituo husika hamhitaji mtumishi huyo