Watumishi wahamishwa bila malipo licha ya agizo rasmi, sheria inasemaje?

MKWANO

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2014
Posts
230
Reaction score
159
Watumishi wamehamishwa kutoka kituo A cha kazi kwenda vituo vingine bila malipo, ingawa agizo la uhamisho lilitolewa na kamati maalumu ya ukaguzi.

Mkuu wa idara, akionyesha nia njema, aliwaita ofisini ili kila mmoja achague kituo cha kazi kwa maandishi.

Hata hivyo, amezitumia barua za kuchagua kituo kuonyesha kuwa tuliomba wenyewe kuhama. Tuna zaidi ya miaka 6 hapa.

Je, tutumie kifungu gani kuomba kulipwa? Bado hatujaripoti, tunasubiri msaada humu. (Local Government)
 
Halmashauri zinazimamiwa na wajinga
 
Pole, ulipaswa ukabidhiwe barua inayokuelekeza kuwa umehamishwa kutoka kituo A kwenda B. Kujiandikia kuwa uende kituo Fulani huo ulikuwa mtego tu, hata hivyo km angekutaka uandike barua ya kujichagulia kituo basi ungemueleza tu kwa mdomo. Huenda hapo kituo cha awali wamewachoka ndiyo maana mnaambiwa mjichagulie pa kwenda. Ungetaja ni Idara gani tungekushauri kwa urahisi njia IPi upitie ili kupata stahiki zako.
 
Mkuu,naomba unishauri na Mimi kuna kitu cha AJABU sana kilinikuta Mimi kuhusu uhamisho.julai 2024 nilihamishwa kutoka kituo N Kwenda kituo E (uhamisho wa kulipwa).nikawa nafwatilia Hela ya uhamisho lakini wapi? October 2024 hela ya uhamisho ikawa umetoka lakini akalipwa mtu mwingine niliyemkuta kituo kipya na hakuwa anahusika na uhamisho,eti walikosea bahat mbaya kwa sababu majina ya Kwanza na ya mwisho yanafanana.
Yule aliyepokea hela kaila na hajachukuliwa hatua na Mimi sijalipwa mpaka sekunde hii.
NAOMBENI USHAURI WENU NIFANYEJE?
 
Pole sana kwa kadhia hio ila itumie kama darasa endapo unaendelea kua mtumishi wa umma chini ya Serikali za mitaa.
Walio elekeza uhamishwe (na/au Muhamishwe) wametumia kanuni kadhaa za kiutumishi (hapa jitahidi uzijue kanuni za kiutumishi wa umma) mfano: mtumishi wa umma anaweza kuhamishwa sababu ya adhabu au kuboresha huduma eneo atakalo enda au mbadala wa aliyekuepo anakoenda pia.
Pia barua uliopewa ya uhamisho imetaja sababu za kikanuni za wewe kuhamishwa kutoka kituo G hadi kituo F.
 
Barua haitaja sababu za kuhamishwa,na hizo barua za kuchagua kituo kwa wote 7 hakuna aliyeomba KUHAMA.
Moja ya jitihada zilizofanyika leo kwenda ofisi ya utumishi kuomba ufafanuzi, hawana jibu na Kaimu Mkurugenzi aliyesaini hizi barua hakujua scenerial,na ameshauri waliporipot kituoni na wàndike barua za malipo.Zikijibiwa ndipo barua za kuomba kuhama zitafutwe
 
Pole, ulipaswa ukabidhiwe barua inayokuelekeza kuwa umehamishwa kutoka kituo A kwenda B. Kujiandikia kuwa uende kituo Fulani huo ulikuwa mtego tu, hata hivyo km angekutaka uandike barua ya kujichagulia kituo basi ungemueleza tu kwa mdomo. Huenda hapo kituo cha awali wamewachoka ndiyo maana mnaambiwa mjichagulie pa kwenda. Ungetaja ni Idara gani tungekushauri kwa urahisi njia IPi upitie ili kupata stahiki zako.
Idara ya Elimu
 
Pole sana kwa kadhia hio ila itumie kama darasa endapo unaendelea kua mtumishi wa umma chini ya Serikali za mitaa.
Walio elekeza uhamishwe (na/au Muhamishwe) wametumia kanuni kadhaa za kiutumishi (hapa jitahidi uzijue kanuni za kiutumishi wa umma) mfano: mtumishi wa umma anaweza kuhamishwa sababu ya adhabu au kuboresha huduma eneo atakalo enda au mbadala wa aliyekuepo anakoenda pia.
Pia barua uliopewa ya uhamisho imetaja sababu za kikanuni za wewe kuhamishwa kutoka kituo G hadi kituo F.
Sehemu J na L ziko upande wa watumishi labda kuwe na waraka unaopinga hivyo vifungu
 
Attachments

Watumishi wamehamishwa kutoka kituo A cha kazi kwenda vituo vingine bila malipo, ingawa agizo la uhamisho lilitolewa na kamati maalumu ya ukaguzi.

Mkuu wa idara, akionyesha nia njema, aliwaita ofisini ili kila mmoja achague kituo cha kazi kwa maandishi.

Hata hivyo, amezitumia barua za kuchagua kituo kuonyesha kuwa tuliomba wenyewe kuhama. Tuna zaidi ya miaka 6 hapa.

Je, tutumie kifungu gani kuomba kulipwa? Bado hatujaripoti, tunasubiri msaada humu. (Local Government)
Hahahaha! Si huwa wanasema uhamisho wa kuomba mwenyewe hakuna malipo. Sasa mlisainishwa bogus treaty walimu wazima, poleni sana.

Walivyowaita ofisini, mlitakiwa mmwambie mwajiri awandikie barua ya kuhamishwa ndio mlipwe.

Lakini hapo kwenye bogus treaty, ngoja waje wataalamu
 
Tayali meza imepinduliwa ,asanteni sana kwa ushauri wenu.
Uhamisho umefutwa kwa sababu ya kukiukwa kwa kanuni na taratibu za kiutumishi.
 
Hapo sawa. Hongereni kwa kujipambania.
Mwl Nyerere alisema "Ukiona msomi anafanyiwa jambo la kijinga bila kuhoji, ujue taifa linatengeneza taifa la wajinga"
 
Back
Top Bottom