kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 18,833
- 23,276
Haya ni mambo yanafikirisha kidogo, kipindi cha shujaa wa Afrika kipenzi cha wana Hayati Magufuli Wananchi walikuwa wakifurika na kutoa malalamiko ya kero zao mbalimbali tofauti tofauti na kuonyesha kuwa zinatatuliwa na wengine kupewa maagizo, na kuona yamepokelewa na kuahidiwa kumalizwa.
Akakaja ndugu Makonda kama katibu mwenezi na staili yake ya kusikiliza kero na kuzitatua papo kwa papo bado idadi ya watu ni kama wale wale na kero ni zile zile na idara ni zile zile na watumishi wanolalamikiwa ni wale wale.
Amekuja waziri Jerry Silaa bado ni vile vile na watumishi ni wale wale waliolalamikiwa kipindi cha Lukuvi, kilichonifikirisha zaidi anakopita Tundu lissu watu ni wale wale.
Amekuja katibu mkuu mpya wa CCM watu ni wale wale, na kichekesho zaidi Makonda alikuwa wilayani akitatua kero na Nchimbi yupo arusha mjini alikopita Makonda silaa wiki tatu nyuma lakini malalamiko ni yale yale na watu ni wale wale.
Swali je watumishi wamejaa viburi hawatekelezi maagizo ya wakubwa wao, au ni maigizo?.
Mama nae alituahidi kila mwezi kukutana na wananchi na kusikiliza kero lakini nafikiri kwa ufinyu wa ratiba imemuwia ngumul akini natumaini watu watarudi wale wale ,je haya ni maigizo ya viongozi wetu?.
Hakuna kama Mama
Twende na Samia 2025!