KERO Watumishi wapya wa Sekta ya Afya katika Halmashauri ya Jiji (Dar) tunafanya kazi katika mazingira magumu

KERO Watumishi wapya wa Sekta ya Afya katika Halmashauri ya Jiji (Dar) tunafanya kazi katika mazingira magumu

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi Watumishi wapya wa Sekta ya Afya katika Halmashauri ya Jiji - Dar es Salaam tunafanya kazi katika mazingira magumu mno.

Tangu tuajiriwe mwanzoni mwa mwezi Novemba 2024, kuna baadhi yetu wamelipwa mshahara wa mwezi November na kuna wengine ambao ni wengine hatukulipwa mshahara wa mwezi huo.

Baada ya kuona wahusika wako kimya na hela hatulipwi tuliamua kwenda kwào kupata mrejesho lakini tuliambiwa sisi ambayo hatukulipwa tulikuwa bado hatujawa approved kwenye mfumo na ndo maana hatukulipwa.

Nimejiuliza sana kwanini pesa inatoka kimafungu na kwanini watu wasifanye hiyo approval ili tupewe haki zetu?

Ni dhahiri kuwa inaonekana kuna uzembe hapo na Serikali inapaswa kufatilia hawa wahusika ikiwezekana wawajibishwe, maana watumishi wenyewe tupo 161 kama sikosei katika Halmashauri ya jiji nzima.

Ukiachana na mshahara pia hata pesa za kujikimu mpaka sasa watu hawajapewa.

Kwa hiyo unakuta mtu hana pesa za kujikimu na Dar hana ndugu, je huyu mtu anaishi katika mazingira gan na anafanyaje kazi?

Tunaomba serikali itusaidie kuhusu hili suala tafadhali kwani uzembe wa baadhi ya watu unafanya watu wengine waishi kwa shida.
 
Pole sana serikali yenu sikivu ipo kazini
 
izo pesa zishaliwa na wajanja

ni sawa na mishahara ya walimu wapya 11,000 inavyotafunwa hapo wizarani wakisingizia mchakato bado
 
izo pesa zishaliwa na wajanja

ni sawa na mishahara ya walimu wapya 11,000 inavyotafunwa hapo wizarani wakisingizia mchakato bado
Kula fweza ni mchakato mkubwa.Haziliwi kama kumbikumbi mkuu.Dokeza kidogo tuone hao vibaka.
 
TULIOAJIRIWA WIZARA YA AFYA OCTOBER.

HATUJALIPWA MSHAHARA WALA KUJIKIMU NA UBAYA TUKO KAZINI.

MZEE KUWA MPOLE MAMBO YANAUMIZA SANA KWA SASA
 
Back
Top Bottom