Watumishi wengi wa Idara ya Afya Wilaya ya Magu hatujapanda madaraja

Watumishi wengi wa Idara ya Afya Wilaya ya Magu hatujapanda madaraja

The wave

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2021
Posts
283
Reaction score
318
Wapendwa nisalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Hapa Magu tumesumbuliwa sana na makatibu wa afya, tumejaza OPRAS mara mbilimbili, tukaombwa barua za ajira, za kuthibitishwa kazini na za kupanda madaraja kwa Mara ya mwisho.

Vyote hivyo tuliwakabidhi, mwezi huu umepita patupu kwa wengi wetu kada ya afya.

Ngoja tuvumilie hadi mwezi unaofuata yaani July. Ukipita patupu kuanzia afisa utumishi hadi makatibu wa afya mjiandae kuachia ngazi kwa uzembe wenu.

Tutapeleka malalamiko kwa katibu mkuu TAMISEMI.
 
Ulivosema Magu, kumbukumbu ikaenda kwa MWENDAZAKE
 
Umenishtua, siku nyingine andika hiyo magu kwa kirefu, halmashauri ya....
 
Ni maeneo mengi hali iko hivyo. Ngoja tuone mwezi ujao nao watakuja na ngonjera zipi. Inakera kufanya kazi zaidi ya miaka sita kwa mshahara ule ule.
 
Take it down a notch mkuu. Ni watumishi wengi bado hawajapanda madaraja. Ni kusubiri tu mwezi ujao.
 
Ni maeneo mengi hali iko hivyo. Ngoja tuone mwezi ujao nao watakuja na ngonjera zipi. Inakera kufanya kazi zaidi ya miaka sita kwa mshahara ule ule.
Kabisa mkuu tena awamu ya mwendazake tulifanya kazi kwa vitisho na kunyanyaswa sana. Nilikuwa na madai yangu nikafuatilia nikajibiwa madai ya zamani hayalipwi Kama hujaridhika acha kazi.
 
Viongozi wa Magu wengi washirikina hivyo hata ukiwatishia tamisemi haikusaidii.

Makatibu wa afya wa hiyo wilaya huwa wana kiburi sana.
 
Viongozi wa Magu wengi washirikina hivyo hata ukiwatishia tamisemi haikusaidii.

Makatibu wa afya wa hiyo wilaya huwa wana kiburi sana.
Kumbe wewe unawafahamu vizuri, wana majibu ya mkato pia wanaona watumishi Kama misukule. Ukiingia ofisini kwao wanakutazama kwa dharau pia majibu wanayotoa unapouliza kitu huwa ya mkato sana.
 
Back
Top Bottom