KERO Watumishi wengi wanahoji kutolipwa Fedha za Kujikimu, mamlaka zipo kimya, hazioni au hazijui kinachoendelea?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Watumishi wa umma wa ajira mpya katika Halmashauri ya Ngorongoro mpaka hivi leo, hatujalipwa kabisa "fedha ya kujikimu" na hatupewi mrejesho wowote na viongozi wetu. Sasa hata hio posho inapoteza maana halisi ya jina "fedha ya kujikimu".

Binafsi ninashangaa sana, watumishi wengi wameibua kero hii, lakini sioni mamlaka inayohusika na malipo kwa watumishi ikitoa tamko au maelekezo maalumu juu ya hizo fedha. Taarifa hizi haziwafikii wizara husika?

Tunaomba hili jambo litazamwe kwa ukubwa, ili kuhakikisha stahiki za watumishi zinawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa
 
Mtawafanya nini pumbavu zenu. Mkiambiwa fight for your rights, mnajikinyata mnamuachia Mange na Maria na Likolola.

Kula chuma .....tena chakavu๐Ÿ˜…๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
 
Jikazeni sio kila siku mnalia lia feza zenu uliambiwa wanazungushia umo kwenye mabenk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ