Watz tumelipa milion 180 alizotafuna mama Mongela Bunge la Afrika

Mmh, Wabunge kama Dr Slaa tunawahitaji wengi sana, kazi bado ni kubwa ya kupambana na ufisadi nchini.
 
Membe alisema pamoja na kwamba, serikali kumlipia madeni Mongella siyo kosa wala dhambi, suala hilo limegubikwa na utata kwani wanaotoa madai hayo hawajafafanua zilikopelekwa fedha hizo kutekeleza malipo hayo.
Kuna taarifa zilishawahi kuripotiwa kuwa huyu Chinga Membe eti anaandaliwa kunyakua kiti kikuu cha Magogoni pale Feri, 2015 . Hapo ndipo CCM ninapowakubali ..wanakata mti wanapanda mti..lol
 
Ndio maana ya maisha bora kwa kila mtanzania. Ukiwa fisadi iba. Serikali itakulipia. Au tuseme ndiyo zilipelekwa Busanda kununua shahada?
 

mmmhh........hii ni kutaka kufunika kombe au?.......kiongozi ukiwa WEAK uwezekano wa pesa kupotea ni Mkubwa.............what else do you want Mr. Membe............
 

Jamani Milioni 180 mali ya walipa kodi kulipiwa Mongella ni kitu kidogo!!!!!!!??? Mmh jamani hata kama ingekuwa ni sent 50 ni mali ya watanzania na lazima tuambiwe ni misingi gani imetumika kulipa hilo deni. Yeye Mongella anatakiwa awajibike kulipa hiyo pesa. Watanzania hawakumtuma kupoteza hizo fedha. Tunahitaji MAELEZO.
 
Membe tunaomba utufanyie kazi bila kulipwa mshahara kucover hilo deni siunasema ni jambo dogo....lipa kwa niaba yetu....turudishieni pesa yetu mheshimiwa membe atalipa deni kwani ni dogo sana kwa mawazo yake
 
 
Huyu Mama inafaa apewqe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine walio (na nia )au wanao lichafua jina zuri la Tanzania...

Wizi hata ukiwa wa senti moja ndani ja jumia ya kimataifa kama bunge la Africa alilokuwa anaongoza huyo mama si jambo la kawaida... Wizi huo kama kweli umethibitishwa umewafanya wawakilishi wa Tanzania katika nchi nyingine wawe watu wa kutiliwa mashaka kama Vibaka ambao hawawezi kuaminika tena katika jumia ya kimataifa...
Pia hata katika ajira, jumia hizi za kimataifa wakiona mtanzania tu... moja kwa moja watakuwa wanakumbuka aliyoyafanya mama Mongera...

Hivyo kama Tanzania haiwakumbatii vibaka wa aina hii, inafaa waioneshe jumuia ya kimataifa kwamba vibaka hupewa Mkong'oto wa hali ya juu sana... sisemi kwamba watu wajichukulie sheria mikoni mwao , but serikali iombe ushahidi kutoka bunge la Africa kwa madai yaliyotolewa dhidi ya mama huyu na apewe nafasi ya kujieleza... kama kuna substance katika mambo anayotuhumiwa basi adhabu kali itolewe na si kuruhusiwa kutumia jina la Tanzania kwa madhamuni chafu anayotuhumiwa kuyafanya...
 
“Nenda ukamuulize Mongella akueleze yaliyomsibu Afrika Kusini. Umuulize kwanini aliamua kuachia Urais wa Bunge la Afrika kabla ya muda wake kufika, atakueleza mambo mengi, lakini hiyo ya serikali kumlipia fedha ni ‘kachembe kadogo’ mno.”

Mheshimiwa Membe hili si suala dogo kama unavyotaka tuamini. Limeleta aibu kwa nchi.Kama nchi iliamua kumlipia basi itakuwa ni kuchekesho cha mwaka. Ina maana kila atakaye kuwa anaiba huko kwenye kazi za nje, serikali ijiandae kuwa inawalipia madeni!!What about credibility ya watanzania kwenye hizo kazi kama kuna scandals za aina hii kwa magwiji wa aina ya mama Mongela?
Jamani, where are our role models? Hawa niliokuwa nawasikia kwa muda mrefu na kuamini wanarepresent tunu bora ya Tanzania,slowly, time has proved me wrong! Kazi kwelikweli
 
Mapinduzi ya kweli, yatalewa wewe na mimi pamoja na sio kuacha kusema wala kusimamia ukweli
 
Tulishasema - Miafrika Ndivyo Tulivyo!

Mkandara:

Waswahili wanasema chembe na chembe ujaza kibaba (kibaba ni sawa la ujazo wa lita moja na zaidi).

Leo Mama Mongella, Jana EPA . Hizo ni pesa nyingi.
 

ONLY in our Tanzania vitu kana hivi vinatamkwa hadharani!

Huyu hana tofauti kubwa na yule bwana mkubwa aliyewahi kutamka kwamba hata ikibidi wadanganyika wale majani, rada ya presidaaa itanunuliwa tu.
 
Hii issue nayo ni RA??

Watanzania mpaka tutakapoona ukombozi ni kuindoa CCM ndio tutaacha kuongea wezi mmoja mmoja!
 
..Benard Membe alikuwa mstari wa mbele kumlipua Dr.Kitine katika ile kashfa ya mkewe kufoji malipo ya matibabu.

..nashangaa ktk hili suala la mama Mongella ameshikwa na kigugumizi.

NB:

..mara nyingi hawa wanasiasa hupigia kelele ubadhirifu/ufisadi kwa maslahi yao binafsi, si kwa maslahi ya taifa. ndiyo maana unaona hakuna constistency ktk hizi kelele zao.
 
..Benard Membe alikuwa mstari wa mbele kumlipua Dr.Kitine katika ile kashfa ya mkewe kufoji malipo ya matibabu.
.

Membe ni Fisadi tu. Ni kauli kama hizi ndo huwa zinawa-cost watu siku za mbeleni - niliwahi kusoma sehemu flani ati huyu Membe naye ni miongoni mwa watu wanaotarajiwa kumrithi kiti JK. Bora his 'true colour' imeanza kunga'ara mapema
 
Sinyolita said:
Membe ni Fisadi tu. Ni kauli kama hizi ndo huwa zinawa-cost watu siku za mbeleni - niliwahi kusoma sehemu flani ati huyu Membe naye ni miongoni mwa watu wanaotarajiwa kumrithi kiti JK. Bora his 'true colour' imeanza kunga'ara mapema

Sinyolita,

..mwandishi alipaswa kumkumbusha Membe jinsi alivyomsakama Dr.Kitine, halafu ndiyo amuulize kuhusu masuala ya Mama Mongella.

..that way mwandishi angemnyima Membe nafasi ya kuleta unafiki na kauli za hovyo hovyo.

..waandishi wetu nao wana matatizo sana jinsi wanavyofanya hizi interviews. inaelekea hawafanyi research ya aina yoyote ile wakati wanaandaa maswali.
 
Sinyolita, waandishi wetu nao wana matatizo sana jinsi wanavyofanya hizi interviews. inaelekea hawafanyi research ya aina yoyote ile wakati wanaandaa maswali.

Yes Jokakuu, waandishi wetu wengi ndo vile tena - no research, not equipped with relevant info/data etc. Wakati mwingine hata wanaweza kuwa wanamuogopa mtu wanayemfanyia interview

Inawezakana pia huyo mwandishi hata hakuwa anafahamu lolote kuhusu issue ya Dr.Kitine

Anyway, Membe hakuwa na sababu ya kusema ati issue iliyomng'oa mama Mongella ni ndogo, isiyopaswa kujadiliwa - issue ndogo isingemgharimu nafasi yake. Na hii ya Serikali kumlipa Mama Mongella hilo deni imekaaje??
 
Membe ni Fisadi tu. Ni kauli kama hizi ndo huwa zinawa-cost watu siku za mbeleni - niliwahi kusoma sehemu flani ati huyu Membe naye ni miongoni mwa watu wanaotarajiwa kumrithi kiti JK. Bora his 'true colour' imeanza kunga'ara mapema
Jokakuu, Kusema kweli mambo kama haya yananishangaza sana kwani sikutegemea kabisa kwamba Membe anaweza toa majibu kama haya.. Kifupi watu wengi humu hawampitishi Membe lakini mimi nilikuwa na matumaini naye sana tu.. sasa napopoona picha kama hii narudi nyuma na kujiuliza huko Bongo kunani? Je, Bongo inabadilisha watu au kuna kitu gani - Fedha, wadhifa au?.
Siamini unajua!
 
Huko ndiyo wanasema kusaidiana kwa kila jambo.. hata kama wananchi watakula majani ili mtanzania mwenzetu asiaibike zaidi.

OMG!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…