Wauaji wa albino kunyongwa Tanzania

Wauaji wa albino kunyongwa Tanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Wauaji wa albino kunyongwa Tanzania
t.gif
20080731162116tombe.jpg

Watu watatu wahukumiwa kifo Mahakama moja iliyopo kaskazini magharibi mwa Tanzania imetoa hukumu ya kifo kwa watu watatu baada ya kumwuua albino.
Watu hao wamehukumiwa kunyongwa kwa kosa la kumwuua mtoto wa kiume albino mwenye umri wa miaka 14.
Walipatikana na kosa ya kumshambulia Matatizo Dunia na kumkata miguu yake katika wilaya ya Bukombe iliyopo mkoani Shinyanga.
Viungo vya albino hutumiwa katika dawa zinazotumiwa na baadhi ya waganga wa kienyeji wakiwaahidi wateja wao kupata utajiri.
Tanzania imeshuhudia ongezeko la mauaji ya albino katika miaka ya hivi karibuni.
Idadi kubwa ya watu wamekamatwa, lakini mfumo wa sheria umekuwa ukifanya kazi taratibu, hii ikiwa hukumu ya kwanza kutolewa.
Kuna kesi nyingine 50 zinazohusu mauaji ya albino katika mahakama za nchi hiyo.
http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2009/09/090923_tz_albino.shtml
 
Back
Top Bottom