Mtu wa kati
Member
- Jul 16, 2022
- 5
- 4
Ni usiku wa manane ambao siwezi kuusahau katika maisha yangu,binti wa miaka kumi na saba akiwa na damu nyingi mapajani alikata roho akiwa wodini,jaribio la kutoa mimba kiharamu lilishindikana na kuamua kuchukua uhai wake na mtoto,lakini chanzo cha yote ni uzembe wa watoa huduma ya Afya kushindwa kumpa huduma na kuanza kumsimanga na kusababisha kifo chake,ndugu na serikali hawana ushahidi lakini chanzo cha hiki kifo ni uzembe wa watoa huduma.
Katika shughuli zake za ujenzi kijana fulani alipata ajali ya kudondoka kutoka juu ghorofani mpaka chini,alipoteza damu nyingi sana kufika kituo cha kutolea huduma za afya hakupata hata huduma ya kwanza iliulizwa fomu ya kutoka polisi PF3 ndio aanze kupata huduma,ndugu na marafiki wakaanza kuangahikia utaratibu wa kupata hizo fomu,hakuna huduma iliyoendelea na mgonjwa kukataa roho baada ya muda mfupi.Wahusika wakiwa na nyuso za kitakatifu wapo kwenye nafasi zao na wala hana hatia yoyote juu ya vifo hivi.
Ndio hapa wengi wetu ni wauaji tusio na hatia kisheria,hakuna mahakama wala jaji atakayeweza kutuhukumu.
Wangapi tumewashauri wapenzi ama wake zetu kutoa mimba kwa kisingizio kuwa hatujajipanga,baada ya ushauri wakatoa mimba na kuja kuwapongeza.Kama wewe ushawahi fanya hivyo na wewe ni muuaji usio na hatia.
Trafiki amepewa mamlaka ya kukagua gari na kusimamia usalama wa raia,lakini kwa rushwa ya shilingi elfu mbili tu ya kitanzania anaacha gari zenye matatizo kuendelea kutoa huduma na kusababisha ajali ambayo inachukua maisha ya watu.
Usipotimiza wajibu wako kwenye kila sekta we ni muuaji usiye na hatia.
Wewe Mwalimu hapo umepewa dhamana kubwa ya kuwafundisha wanafunzi wako,unaacha majukumu yako ya msingi ya kufundisha na kutengeneza wasomi vimeo wanaosababisha vifo kwa watu wengine nawe pia ni muuaji usio na hatia.
Kaa chini jitafakari kwa makini je wewe ujawahi kumuuwa mtu kwa makusudi ama bahati mbaya.
Unaweza sema hapana lakini kama hujawahi timiza wajibu wako kwa asilimia mia moja ni lazima tu umewahi kuua.
Wewe Mwananchi wa kawaida ulipata nafasi katika sanduku la kura ukachagua kiongozi asiye na sifa anayekula rushwa na kusababisha ubovu wa huduma na urasimu na kusababisha vifo kwa namna moja ama nyingine nawe ni muuaji kama wauaji wengine.
Ni kawaida ya binadamu kujiona bora kuliko wengine lakini wapo pia viongozi wa dini wanawatoa wagonjwa mahututi hospitalini na kwenda kuwaombea kwa magonjwa yanayoweza kutibika hospitalini huo ni uuaji pia.watu wengi wamekufa lakini hakuna mahakama wala jaji atakuhukumu.
Dereva umelewa unaendesha chombo cha moto kwa spidi ya hatari na kusababisha ajali kwa watu wewe pia ni muuaji usiye na hatia.
Na wewe mhandisi unatekeleza miradi chini ya kiwango na kusabisha majengo kuporomoka,maji kutotoka na barabara zisizo na viwango pia wewe ni muuaji pia usiye na hatia kisheria.
Hakuna kundi la watakatifu ambalo halina hatia katika hili,kuna watu wanakufa na njaa,lakini una bando la kuperuzi kutwa nzima katika kurasa za ngono, umbea hata humu JF wakati ungeweza kusaidia hicho kidogo kwa watu wasiojiweza kupata angalau chakula tu.
Kikubwa ni kutimiza wajibu na kuwajibika kwa kiwango kikubwa tu, ni kweli kifo ni mpango wa mungu lakini usiwe sababu ya kuwa chanzo cha hivyo vifo,kikubwa tujitafakari kwa kila mtu kwa nafasi yake ili tusiwe chanzo ya vifo vitokanavyo na uzembe wetu wa kuwajibika,kila mtu atimize wajibu wake na kutenda haki ili dunia iwe salama kwa binadamu wote.
Alamsik

Upvote
2