Wizara ya Afya Tanzania
Official Account
- Oct 1, 2020
- 58
- 127
Wauguzi na Wakunga wametakiwa kuwasimamia wauguzi na wakunga watarajali (interns) waliopo mafunzoni kwa vitendo na kuhakikisha wanafundishwa vizuri ili kuweza kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ziada Sellah alipokuwa akizungumza na wauguzi na wakunga katika Mkoa wa Lindi.
"Interns hawa tuliowapata tuwasimamie kwenye kazi zao, tusiwaache wafanye kazi peke yao" amesema Bi. Ziada kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.
Amesema wagonjwa wanatakiwa kupewa huduma bora ambazo kwa asilimia kubwa wakiwa hospitalini huwa wanahudumiwa na wauguzi hivyo si sahihi 'interns' hao wakiachwa peke yao kuwahudumia wagonjwa.
Aidha Bi. Ziada amewataka watarajali hao kuwaheshimu wakufunzi wao ambao ni wauguzi na wakunga wenye uzoefu wa kutosha ili waweze kujifunza vizuri na kuweza kutoa huduma nzuri.