Wauguzi wa Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar wasimamishwa kazi kupisha uchunguzi baada ya Mama kujifungulia chooni

Wauguzi wa Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar wasimamishwa kazi kupisha uchunguzi baada ya Mama kujifungulia chooni

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wauguzi katika Hospitali ya Wazazi Mwembeladu Zanzibar wamesimamishwa kazi kwa muda wa wiki mbili ili kupisha uchunguzi kufuatia mama kujifungulia mtoto chooni baada ya kupata uchungu akiwa hospitalini hapo kwaajili ya kujifungua.

Hata hivyo inadaiwa kuwa akiwa hospitalini hapo wauguzi wa zamu walimtolea maneno ambayo hayakuwa rafiki wala faraja wakati akiugua uchungu na hata alipojifungua walimtaka mama huyo asafishe pale alipojifungulia mtoto wake.

Je, unafikiri nini kifanyike ili kuondoa manyanyaso kwa wajawazito wanapokwenda kujifungua katika vituo vya afya?

Hivi kwanini michezo na tabia chafu zinaendelea kujitokeza kwa baadhi ya wauguzi katika hospitali au tuseme sheria ni nyepesi?

Soma Pia:
Maana inatisha matukio kama kuendelea kutokea kila kukicha kutoka kwa wauguzi
 
Wafukuzwe kazi vipi kama uyo mama angepoteza maisha na mtoto wake
 
Majina ya Zanzibar yanafurahisha sana
Mwembeladu, Skuli ya Dole, Mchambawimba, Kizim mkazi, Mfereji Malingo, Halikuniki etc.
 
nashindwa kuelewa hawa wauguzi wa hizi hospitali za serikali hapa nchini huwa wanasumbuliwa na nini, hizi kesi ni za kila siku. Hao ni wakuwatimua tu iwe fundisho kwa wengine.
 
Back
Top Bottom