Waumini Uganda wamshukuru Mungu kwa kufukuza Ushoga

Waumini Uganda wamshukuru Mungu kwa kufukuza Ushoga

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Raia wa Uganda kutoka dini mbali mbali hii leo wamekusanyika katika uwanja wa Kololo mjini Kampala kwa maombi maalum ya kumshukuru Mungu, na kutoa shukurani kwa Rais Yoweri Museveni kwa kutia saini mswaada wa sheria unaozuia mapenzi ya jinsia moja.

Viongozi wa dini mbalimbali wakristo na waislamu wamehimiza waumini wao kujitokeza kwa wingi katika ibaada hiyo maalum.

Hii ni mara ya kwanza viongozi wa dini mbali mbali nchini Uganda kujitokeza kwa pamoja na kuandaa Ibaada maalum ya kumshukuru Rais Museveni na kuliombea taifa kuepuka vitendo vya ushoga.

Rais Museveni aliidhinisha sheria hiyo ambayo raia wengi wa Uganda wameipigia debe sana.
Ibaada hiyo maalum inafanyika uwanja wa uhuru wa Kololo mjini Kampala, baada ya karibu mwezi mmoja na nusu tangu rais Yoweri Museveni kuiidhinisha

Tangu Rais Museveni kuidhinisha sheria hiyo kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mataifa ya Magharibi yakimtaka kubadili msimo wake, huku baadhi ya mataifa yakipunguza msaada kwa Uganda.
Lakini raia wengi wa Uganda walimsifu Rais Museveni kwa hatua yake.

BBC
 
Tanzania viongozi wetu hawezi kupinga ushoga kama alivyofanya M7, sababu viongozi tulionao ni wazururaji wazuri kwenye hizo nchi zinazo hubiri Ushoga.
 
jamani si walete hiyo sheria Tanzania sijui kinachoshindikana ni kitu gani
 
Safi sana, Jamani na sisi Tanzania tuupinge kwa nia moja...
 
Back
Top Bottom