PostGE2025 Waumini wakusanyika nje ya kanisa la Askofu Gwajima

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Kutoka Ubungo -Chai bora, jijini Dar es Salaam yalipo makao makuu ya Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo chini ya Askofu Dkt. Josephat Gwajima, Jambo TV imepita na kushuhudia baadhi ya waumini wa Kanisa hilo wakiwa wamejitokeza kwenye viunga vya Kanisa hilo mchana wa leo, Jumanne Novemba 25, 2025

Taarifa zinaeleza kuwa waumini hao wamejitokeza kwenye viunga hivyo kufuatia agizo lililotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye Novemba 24, 2025 alimuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuhakikisha wanalifungulia Kanisa hilo, ili waumini wake waendelee na ibada huku likiwa kwenye uangalizi maalum, agizo lililoenda sambamba na 'nyumba' nyingine za ibada

Jambo TV imepata taarifa kuwa muda wowote kutoka sasa wawakilishi wa serikali watafika kwenye viunga hivyo na kuzungumza na waumini hao kwaajili ya kuwapa muongozo


Your browser is not able to display this video.
 
Wangetulia tu, yaani serikali ndiyo inaaamuru Mungu aabudiwe au asiabudiwe. Tena kwa muda gani!

Hii Tanzania imekuwa channel ya vichekesho huko ughaibuni
Mungu yupo kanisani tu?
 
Miungu Watu wamelisamehe Kanisa.
 
Hii issue kila wanapokanyaga ni moto, watu hawataki amani tena wanataka haki tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…