Waungwa nisaidieni, mtoto wangu ana miaka 3 sasa lakini haongei wa hawezi kula mwenyewe

Waungwa nisaidieni, mtoto wangu ana miaka 3 sasa lakini haongei wa hawezi kula mwenyewe

Joined
Jan 9, 2014
Posts
13
Reaction score
3
Heshima kwenu wote,
Mimi na mke wangu hatuna furaha kabisa kutokana maendeleo ya mtoto wetu. Mpaka sasa hivi ana miaka 3 ajabu hawezi kuongea wala kula mwenyewe.Chakula analishwa na anakula vizuri, kama akiwa na njaa sana na chakula kikawekwa chini tayari kwa kuliwe,yeye husogea pale na kuanza kula kwa mdomo na sisi kama wazazi wake tunachofanya ni kumpiga ili asizoee tabia hiyo.

Kwa kweli yeye mwenyewe ni mjanja na mchangamfu anapenda sana kutembea usipo mwangalia vizuri huwa mara nyingi anatutoroka nyumbani.

Wakati anazaliwa alizaliwa kwa matatizo, yaani alichelewa kuzaliwa, ilitakiwa mama yake aende thieta kwa ajili operation kutokana na kushindwa kazaa katika njia ya kawaida, lakini kabla maamuzi rasmi hayajatolewa dactari alikuja na akasema mke wangu anaweza akazaa kawaida bila kwenda thieta isipokuwa ataongezwa njia tu.

Mchakato wa kumwongeza njia ulifanyika na hatimae mke wangu akajifungua mtoto.Yule mtoto wakati anazaliwa hakulia akapigwa mabao sana kisha akaanza kulia,pia aliwekwa kwenye oven lile la watoto.

Kutembea pia amechelewa sana, ameanza kutembea akiwa na miaka 2.1 kwa sasa anatembea tu vizuri. Tatizo liko kwenye uongeaji na ulaji. Mikono yake iko vizuri tu,vitu anavyopenda yeye kunyanyau huwa ananyanyua kwa mikono yake lakini ukimshikisha kitu huwa ataki kabisa kushika,ukimlazimisha analia.

Naombeni msaada wenu nifanyeje juu ya huyu mtoto maana mtoto mwenyewe ni wa kwanza hatujui chochote mpaka tunachanganyikiwa.

Asanteni sana
 
Heshima kwenu wote,
Mimi na mke wangu hatuna furaha kabisa kutokana maendeleo ya mtoto wetu. Mpaka sasa hivi ana miaka 3 ajabu hawezi kuongea wala kula mwenyewe.Chakula analishwa na anakula vizuri, kama akiwa na njaa sana na chakula kikawekwa chini tayari kwa kuliwe,yeye husogea pale na kuanza kula kwa mdomo na sisi kama wazazi wake tunachofanya ni kumpiga ili asizoee tabia hiyo.

Kwa kweli yeye mwenyewe ni mjanja na mchangamfu anapenda sana kutembea usipo mwangalia vizuri huwa mara nyingi anatutoroka nyumbani.

Wakati anazaliwa alizaliwa kwa matatizo, yaani alichelewa kuzaliwa, ilitakiwa mama yake aende thieta kwa ajili operation kutokana na kushindwa kazaa katika njia ya kawaida, lakini kabla maamuzi rasmi hayajatolewa dactari alikuja na akasema mke wangu anaweza akazaa kawaida bila kwenda thieta isipokuwa ataongezwa njia tu.Mchakato wa kumwongeza njia ulifanyika na hatimae mke wangu akajifungua mtoto.Yule mtoto wakati anazaliwa hakulia akapigwa mabao sana kisha akaanza kulia,pia aliwekwa kwenye oven lile la watoto.

Kutembea pia amechelewa sana, ameanza kutembea akiwa na miaka 2.1 kwa sasa anatembea tu vizuri. Tatizo liko kwenye uongeaji na ulaji. Mikono yake iko vizuri tu,vitu anavyopenda yeye kunyanyau huwa ananyanyua kwa mikono yake lakini ukimshikisha kitu huwa ataki kabisa kushika,ukimlazimisha analia.

Naombeni msaada wenu nifanyeje juu ya huyu mtoto maana mtoto mwenyewe ni wa kwanza hatujui chochote mpaka tunachanganyikiwa.

Asanteni sana
imetokea kwa mtoto wangu wa kwanza pia yeye alitembea karibu miaka 2 lakini kuongea pia alichelewa amefika miaka 3 pia haongei kila hospital tulimpeleka wakasema ana matatizo ya mishipa kuchelewa kukua kuendana na umri wake so kila kitu atachelewa now anamiaka 8 kweli ile hali bado naiyona pamoja na kua na miaka 8 utasema anamiaka mi 5 amebidi aanze darasa la kwanza na miaka 8.

so hayo ni majaliwa tu ushukuru mungu sio tahira mybe pia anaweza kubadilika baadae kama mimi ninavyoambiwa
 
Jaribu pia kumpeleka sehemu za mchanganyiko na watoto wenzake, usipende kua nae mara kwa mara.

Huko atacopy mambo mengi toka kwa wenziwe maana atajitahidi kufanya kama wanavyofanya wenzake kucheza,kuongea,kuimba,kula n.k
 
Mkuu kama hana tatzo la akili na yupo poa ni kuvuta subra tu ila muhimu ni umchanganye na watoto wenzie akajifunzie huko na umtafutie na mdogo wake kabsa.....

Ukuaji wake upo slow huyo...
 
Hiyo ni celebral palsy..jaribu kumpeleka kwenye speech therapy na mchanganye na watoto wenzie..ataongea tu usijali...binafsi niko kwenye changamoto kubwa kama hiyo.

mi mwanangu aliumwa homa ya uti wa mgongo leo katimiza mwaka na miezi nane hawezi kukaa bado..pia Maombi muhimu tuwaombee sana, Mungu aliyetupa anamajibu
 
Back
Top Bottom