Waungwana nauliza nini maana ya msukule au mtu kuitwa msukule?

Waungwana nauliza nini maana ya msukule au mtu kuitwa msukule?

msumeno

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2009
Posts
2,826
Reaction score
1,734
Naombeni kujuzwa maana halisi ya MSUKULE.... Au kitu au ili mtu aitwe MSUKULE inabidi aonekanaje au au awe na matendo yepi.....ni hilo tu
 
Naombeni kujuzwa maana halisi ya msukule.... Au kitu au mtu aitwe msukule inabidi aonekanaje au au awe na matendo yepi.....ni hilo tu

ni nick name ya wanachadema hapa jukwaani una jingine
 
Msukule ni binadamu aliye zaniwa kufa kumbe anaishi katika ulimwengu wa kichawi. Anakuwa ndiye kiumbo ila akili zake zinakuwa zimelengwa kutambua yale anayo amliwa na mabwana zake tu. Hajui ndugu zake wala hajitambui yeye mwenyewe ni nani na anatoka wapi. Mtu ambae hajawahi kufa na kuzikwa huwezi kumuita msukule, ni tusi.
 
Wewe mkuu usipate shida nenda kalale makaburini tu utaona tofauti ya msukule na binadamu.
 
kama walivyoelezwa na wajumbe.lakini kwa jf mana yake ni kada wa chama asiyejitambua,amekabidhi akili zake kwa Nape na kutumikishwa kutwa humu.MSALANI ni mfano mzuri
 
Wewe mkuu usipate shida nenda kalale makaburini tu utaona tofauti ya msukule na binadamu.

Wala asipate shida yakwenda makaburini aende pale lumumba atawakuta vijana wengi natsht zao za kijani zenye maandishi chagua kikwete na maisha bora kwa kila mtanzania.
 
KWA TAFSIRI YA KISIASA KWA MUKTADHA WA TANZANIA: msukule ni mtu yeyote anayetetea kwa nguvu sana siasa zote chafu zinazofanywa na CCM dhidi ya umma wa walala hoi wa nchi hii.
 
Ukitaka kujua tabia za msukule mtazame Nape. Alikuwa kiongozi kwenye UVCCM. Kule akatofautiana na Lowasa kwa kumwita ni fisadi. Alimwudhi Kikwete kwa kumpigia kampeni Baba yake (Prof. Mwandosya). Yeye Nape, akagangamala akisema hatasalimu amri, atagombea na cheo cha juu kabisa cha UVCCM. Kikwete na Lowasa wakaamua kummwua Nape (kisiasa). Baadaye wakamrudisha akiwa msukule. Tangu aliporudishwa hakumbuki chochote katika vile alivyokuwa akipigania. Leo anazunguka nchi nzima akimsifia Kikwete na Lowasa.
 
Ukitaka kujua tabia za msukule
mtazame Nape. Alikuwa kiongozi kwenye UVCCM. Kule akatofautiana na
Lowasa kwa kumwita ni fisadi. Alimwudhi Kikwete kwa kumpigia kampeni
Baba yake (Prof. Mwandosya). Yeye Nape, akagangamala akisema hatasalimu
amri, atagombea na cheo cha juu kabisa cha UVCCM. Kikwete na Lowasa
wakaamua kummwua Nape (kisiasa). Baadaye wakamrudisha akiwa msukule.
Tangu aliporudishwa hakumbuki chochote katika vile alivyokuwa
akipigania. Leo anazunguka nchi nzima akimsifia Kikwete na
Lowasa.

Kumbe Kinana anazunguka na msukule......!!!?
 
Msukule ni binadamu aliye zaniwa kufa kumbe anaishi katika ulimwengu wa kichawi. Anakuwa ndiye kiumbo ila akili zake zinakuwa zimelengwa kutambua yale anayo amliwa na mabwana zake tu. Hajui ndugu zake wala hajitambui yeye mwenyewe ni nani na anatoka wapi. Mtu ambae hajawahi kufa na kuzikwa huwezi kumuita msukule, ni tusi.

Mkuu umesahau kutoa mfano. Mfano mzuri ni wale jamaa zetu wa lumumba kwa jina maarufu la watoto wa interahamwe
 
Wala asipate shida yakwenda makaburini aende pale lumumba atawakuta vijana wengi natsht zao za kijani zenye maandishi chagua kikwete na maisha bora kwa kila mtanzania.

Mkuu naona hapo umemaliza majibu yote cdhani kama kuna majibu sahihi zaidi ya haya
 
Kwahiyo Misukule ndo Nterahamwe hao hao....du kweli kiswahili kigumu aisee
 
Misukule kwa gwajima wapo aende atawaona ni kanisa la ufufuo na uzima nadhani lipo kawe
 
Naombeni kujuzwa maana halisi ya MSUKULE.... Au kitu au ili mtu aitwe MSUKULE inabidi aonekanaje au au awe na matendo yepi.....ni hilo tu

Isaya 42:22 inaelezea kwa habari ya watu walioibiwa na kutekwa, watu waliofichwa katika magereza. Kimsingi msukule ni yule mtu alieibiwa na kufichwa mahali na kutumika sawasawa na kusudi la mwivi mwenyewe.

Kuna aina nyingi za misukule, nitazielezea chache:
1. Mtu anafariki anazikwa, ambaye kimsingi siku zake za kufa hazikufika ila wachawi wamemchukua na kwenda kumtumikisha

2. Mtu mnaishi nae, lakini roho yake imeibiwa inafanya kazi mahali, kwahiyo huyu mtu anakuwepo mnaishi naye lakini ndani yake amewekewa roho ya jini ambayo ndio inafanya huo mwili uishi maana imeandikwa mwili bila roho umekufa. Hawa watu wanakuwa na tabia fulani ambazo haziko sawa, kama ni mwanafunzi alikuwa anakuwa wa kwanza darasani anashuka mpaka hata kuwa wa mwisho, mtu umeajiriwa sehemu unalipwa 2000 kutwa nzima na wewe unajionea sawa tu, mambo yako yanaharibika, inakywa tofauti na ulivokuwa mwanzo!

Hiyo ni kifupi tu ila kuna vitu vingi na dalili nyingi sana, ambapo ukienda kawe Ufufuo na Uzima unaweza ukapata DVD za dalili za mtu aliechukuliwa msukule
 
Back
Top Bottom