Wauswazi wenzangu, mnakumbuka matani? Twende, twendee, twendeee

Mikono mirefu hadi unaomba chenji kwenye ndege
Mdomo mkubwa vitumbua unakula kama karanga
 
Kichwa kikubwa utafikili diaba la maji.twendetwendeee.ila mi ilikuwa sipendi coz some yalikuwa ya kweli.
 
Twende twendee kichwa kama tofali!!
Twendee twendeee mpana kama pazia la sinema.....!kwa vile nilikuwaga kitoto flan kineneeee nikishapewa hii naachia bonge la kilio lol!
 
hatutaki mabezo,mwenye nguvu apute....haya nilipe ng'ombe wangu.
 
Pua kama ncha ya bamia!.........macho kama fundi saa kapoteza nati
 
Mdomo kunuka ushuzi wa bubu!
Kidevu ka ngazi ya uda!
 
Twende twende.... Kichwa kikubwa Kama mabeewa ya treni
 
Twndeee........ Mweusi kama mafuta ya bunduki. ( hadi leo sjayaona mafuta ya bunduki yalivyo)
 
nini! nini! nini!
Nywele kaa mkutano wa nzi, twende,twende, ulisikia sikukuu ya watoto ukavaa nepi, ****** juu juu kaa breki ya fire.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…