Mi binafsi nawakubali sana Bongo Flava, ni moja ya sehemu chache ambazo nimetokea kuelewa burger zao na bei ni reasonable tu. Sema tatizo nadhani lipo zaidi kwenye ishu ya location.
Walitakiwa wa-target sehemu ambayo tayari ina mikusanyiko ya watu maana mara nyingi watu wanapendwa kwenda sehemu ambayo anaweza akapata huduma zaidi ya moja. Kama KFC ya Mlimani City, that place is ALWAYS packed. Na sababu kubwa ni kwamba watu wanaenda shopping, kucheki movie, watoto kucheza na wanaunganisha kula huko huko.
Sasa BF even though nawakubali sana ila siwezi kula chakula chao unless nna mishe mishe maeneo ya Kariakoo, kitu ambacho sio cha mara kwa mara. Wala siwezi kufunga safari mpaka Sinza kisa tu burger 1 au 2. Mwenye nayo ajaribu kujifikiria zaidi kwenye swala la location, a-invest kwenye location ambayo itamrudishia hela yake. Yani bora awe na sehemu moja yenye wateja wengi kuliko sehemu kibao zenye wateja wa kubangaiza.