Wauza mboga mnaotembeza kwenye madishi mnasumbua kwa hodi alfajiri sana

I AM NO ONE

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2020
Posts
389
Reaction score
576
Za asubuhi members,

Jamani kuna haka katabia kakuletewa mboga nyumbani na wale wakina mama wajasiriamali; ni vyema wanapata hela na riziki lakini kuna tabia mtu anapiga hodi utasema anakudai kwa lisauti likubwa zito utasema sasa imekuwa ugomvi au nini.

Sasa mbaya zaidi ndiyo muda ambao unakuta mtu ndiyo upo na mkeo au demu wako.

Mnaoishi nao naomba muwape taarifa sio vizuri, wabishe hodi taratibu na muda wa kuuza mboga sio saa kumi na mbili kamili asubuhi, bado mapema sana hata mtu hujatoka kitandani aise na hujapanga kitu chochote.
 
Hao dawa ni kuwachunia tu wanaacha wenyewe, kuna mjinga alikuwa anakuja home kila asubuhi "wenyewe wenyewe" dah inakera!
 
Saa ngapi,kama ni saa kumi alfajiri kweli ni kero,,lakini saa tano asubuhi sio kero
 
Mh sasa wale kina mama wapo humu mkuu!? Huu ujumbe utawafikia kweli?
 
Za asubuhi members,

Jamani kuna haka katabia kakuletewa mboga nyumbani na wale wakina mama wajasiriamali; ni vyema wanapata hela na riziki lakini kuna tabia mtu anapiga hodi utasema anakudai kwa lisauti likubwa zito utasema sasa imekuwa ugomvi au nini.

Sasa mbaya zaidi ndiyo mda ambao unakuta mtu ndiyo upo na mkeo au demu wako.

Mnaoishi nao naomba muwape taarifa sio vizuri, wabishe hodi taratibu na muda wa kuuza mboga sio saa kumi na mbili kamili asubuhi, bado mapema sana hata mtu hujatoka kitandani aise na hujapanga kitu chochote.
Badala ya kwenda kununua mboga za majani sokoni nyinyi mnapenda vya urahisi kuletewa mpaka mlangoni, ndio maana mnawekewa sumu na wagomvi wenu mnakufa bila kujijua. Utawekaje mazoea na mtu wa barabarani kuwa anakuletea mboga kila siku?
 
hujaelewa mkuu kabisaa umekurupuka .... soma ulewe complaints zangu
 
Yani umeshindwa kuwaambia wenyewe hadi uleteuzi humu!!.

Humu kunawauza mboga??
 
hujaelewa mkuu kabisaa umekurupuka .... soma ulewe complaints zangu
Nimekuelewa vzr, hv muuza mboga atawezaje kuja kugonga kwako bila ya wewe kuwa na tabia ya kununua hizo mboga. lazima akuamshe mteja wake
 
Death is everywhere ukanunue mboga urafik kariakoo sokoni ,hizi mbogo tunanunuaga toka miaka niko mtt mpka leo na maisha yanendelea tu mkuu.
 
Kwahiyo umeshindwa kuwaambia unakuja kututuma sisi tukawaambie? Acha watu watafute rzk za halali achen kuvimba hii Ni dunia
 
Hao dawa ni kuwachunia tu wanaacha wenyewe, kuna mjinga alikuwa anakuja home kila asubuhi "wenyewe wenyewe" dah inakera!
mimi nachunaga kabisaaaaaaaa yan na leo nimempa makavu nikamwambia dah mbona mapema ivo leo
 
Yani mtu anatafuta ridhiki yake kwa jasho lake ww unachukia...ungejisikiaje ww unaenda sehem kuomba kazi halafu wanakutimua hata usikaribie tena hilo eneo..
 
Back
Top Bottom