Hvi wadau kuna Samsung J7 duo ambayo nyuma ina kamera mbili,so mwnye uelewa naomba anipe kazi ya zile kamera maana ,kuna moja ukiiziba unapga picha kama kawa bt ukiziba ile nyingine hupat picha.
Hio ambayo ukiziba hupati picha ndio primary camera na hufanya kazi zotee, km viewing/focus, zooming, sensing, capturing the light, shooting, depth, n.k n.k
hio ambayo ukiiziba huoni effect yoyote ndio secondary, hii ni kwaajili ya kuboresha ubora wa picha hasa kwa kufanya zooming, colour sensor(black and white only) na sensor depth.
ukiona hivyo ujue simu unayotumia zina share same light receiver.
kinachotokea ni kwamb hizo 2 cameras with 2 lens zinachukua 2 beams of light, zinapeleka kwenye 2 sensors(zenye sifa mbili tofaut) ambazo zitafanya convertion kwenda kwenye electronic signal then sasa zinaunganishwa kutengeneza image moja yenye quality nzuri halaf inatumwa kwenye receiver ikiwa kama single image na wewe utaona picha kulingana na UWEZO WA MACHO yako,
kwa nini hii teknolojia ya multiple camera imekuja kipnd hk? Ni katka kufanya smartphone kua simple object inabd iwe ndogo hasa nyembamba kitu ambacho kinaathili sana battery na camera, ukipunguza upana wa simu means unapunguza ukubwa wa sensor na lens yake, kumbuka lens kazi yake ni kuchukua mwanga kutoka nje na kuutuma ndan kwenye sensor ambayo ita sense object iliyopo kwenye ule mwanga na kutengeneza pixels kulingana na wingi wa mwanga ulioingia, kwa ufup kamera ikizid kua fupi unapunguza ubora wa picha itakayo tengenezwa, hii ni concept ya physics specificaly light, ila hapa naweza kukupoteza kbsa maana kuna ups and down nying sana, kama kipnd kile mwl anafundisha light akawa anakucholea zile cross cutting anakuambia hii ni object, hii ni focal point, hii ni focal length, hii ni image sensor na mirror n.k n.k wewe unamng'ong'a kisogoni huku unakula mabumunda, haki hutonielewa, ila usihof ngoja nitumie simple concept ya single eye or two eyes utanielewa tu.
Hebu njoo hapa chini,
Ushawahi kupiga picha huku kabla hujacapture ile image ukazoom kwanza ili uone object kwa ukaribu/ukubwa? kama ndio basi hio inaitwa digital zoom, na haina tofauti hata kidogo na mwingine alieamua kupiga picha kwanza ndio akazoom, ukifanya hivi ujue umekuza image au umeisogeza karibu ila umeipunguza quality, km huamin piga picha nenda kwenye details/properties usome resolution na pixels halaf zoom/crop then angalia tena ubora wa picha na ukubwa wa resolutio na pixels, sasa kutatua hili tatizo ndio wanaweka camera ya pili kwa ajili ya zooming tuu bila kuharb ubora wa pics, na inafanya kazi panapo ulazima tuu, sehemu ambayo haijafocuss object yyt ya kuzoom basi hutaona ikifanya kazi baadala yake kazi zote zitafanywa na primary camera na pia haiwezi kufanya kazi sehem yenye mwanga mdogo, wewe utaweza uone mwanga ni mkubwa lakn sensor zake zinakataa baadala yake itasaidiana na primary ku trap light na sio kuzoom,
Pili inaweza kutumika kama depth sensor, hembu fanya hili jaribio hapo ulipo.
haya haya maandishi unayo yasoma elekeza macho sehemu moja, pale ulipoelekeza macho kile kitu lets say ni HAPA utaona hilo neno very clear ila ya pembeni utaona km yamefifia hv au km ukungu hivi kadiri umbali unavyoongezeka, hii ndio dual camera,
hembe sasa funga jicho moja halaf rudia hilo zoezi....., hapa hilo tatizo halitajitokeza ila utakua umepunguza uwezo wa kuona eneo kubwa, hii ndio single camera.
na ukilazmisha macho yote yaangalie neno moja itafka wakat na hlo neno hulion vzr, ndio maa na kwenye simu ile autofocus ukiwa unapga picha inakuja na kupotea, huwez lazmisha camera nzima mda wote ifocus tuu,
kinachotokea hapo juu km hujui, ni kwamba unapotaka kuangalia kitu kwa umakini uone details zake vizuri, automatica jicho moja lina focus targeted object na jingine linaua backgroud isiathiri sensor ya jicho la pili, ukifunga jicho moja ni kwamba utakua umekuza ile targeted point yako ila ukubwa wa eneo kwa ujumla umeupunguza, lengo la camera mbili ni kuleta ushirikiano ku produce better image, km simu ina camera 4 kma samsung a9 au 5 km nokia 9 halaf hazina ushirikiano ni sawa na watu elf moja wenye speed moja wote kumkimbiza mbwa koko halaf watarajie kumkamata kwa kigezo cha wing wao,
kwaio ile camera ya pili haiwez kufanya kaz bila ya kwanza, na wewe hata kidogo huwez ukaicontrol mda gan ifanye kazi na mda gan isifanye, inafanya kazi pale tu primary camera inapohtaj msaada au kulingana na mwanga uliopo mda huo, na pia inaweza ifanye kazi flan lakn wewe hukugundua kutokana na uwezo UWEZO WA MACHO yako.
nimechoka hata sielew ninachoandika tena, nalala nitaendelea kesho, km una swali ulizaaa