Wauzaji wa bidhaa wa Rwanda kutafuta fursa kwenye maonyesho ya CIIE mjini Shanghai

Wauzaji wa bidhaa wa Rwanda kutafuta fursa kwenye maonyesho ya CIIE mjini Shanghai

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
Kampuni kadhaa za Rwanda, zilishiriki kwenye maonyesho ya saba ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa za China (CIIE) yaliyofanyika mjini Shanghai.

Maonyesho hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Biashara ya China kwa kushirikiana na Shirika la Biashara Duniani (WTO), ni maonesho makubwa zaidi ya kuagiza bidhaa kutoka nje na yamekuwa ni jukwaa kubwa la ununuzi wa kimataifa na kuhimiza uwekezaji.

Rwanda imekuwa ikishiriki kwenye maonyesho hayo tangu yalipozinduliwa mwaka 2018, na kuhimiza watumiaji wa China kuzifahamu bidhaa za Rwanda, pamoja na kutafuta fursa za uwekezaji.

Kwa mujibu wa ubalozi wa Rwanda nchini China, kampuni za Rwanda zilizoshiriki katika CIIE ya mwaka huu ni pamoja na zile zinazotangaza kahawa, pilipili, asali na sanaa za mikono.
 
Sisi tuko busy na kuchakachua uchaguzi wa serekali za mitaa.
 
Back
Top Bottom