BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete amesema wanachukua hatua hiyo ili kulinda Mazingira na Kunusuru vyanzo vya Maji.
Amesema wale ambao watafuatwa kwenye maeneo yao, Serikali itawafidia lakini hawatakuwa tayari kuona ukame ukiendelea katika Mabonde hayo.
Ridhiwani ameongeza kuwa operesheni hiyo itafanyika vizuri licha ya upotoshaji unaoendelea akieleza kuwa bonde hilo limekauka kutokana na shughuli za kijamii na kwamba watawaondoa wote waliovamia maeneo hayo.
=====================
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema katika kulinda mazingira na kunusuru vyanzo vya maji haitasita kuwaondoa wananchi waliovamia bonde la Ihefu na Songwe na kwamba wale waliofuatwa watalipwa fidia.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Novemba 16 na Naibu Waziri wa wizara hiyo Ridhiwani Kikwete wakati akitoa salamu za wizara hiyo kwenye mkutano Mkuu wa nane wa mwaka wa bodi za maji za mabonde unaofanyika jijini hapa kwa niaba ya Waziri Dk Angelina Mabula.
Mkutano huo ambao umehusisha wadau mbalimbali umekutanisha wizara za kisekta ikiwamo Wizara ya Maji, Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Nishati, Madini, Kilimo na Uvuvi Tamisemi n Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mikoa kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ambaye ndiye mgeni rasmi.
Ridhiwani amesema operesheni inayoendelea itafanyika vizuri licha ya upotoshaji unaoendelea akieleza kuwa bonde hilo limekauka kutokana na shughuli za kijamii na kwamba watawaondoa wote waliovamia maeneo hayo.
Amesema wale ambao watafikiwa serikali itawafidia kwa utaratibu lakini hawatakuwa tayari kuona ukame ukiendelea katika mabonde hayo na kuhatarisha maisha ya wanadamu.
"Niwatoe hofu wananchi kwamba shughuli itafanyika vizuri waliovamia maeneo hayo wataondolewa na waliofuatwa watafidiwa kwa utaratibu japokuwa upo upotoshaji ambao hatutaupa nafasi" amesema Mbunge huyo wa Chalinze.
Ameongeza kuwa katika bajeti ya Sh 50 bilioni zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya Halmashauri zote nchini, tayari Sh4.75 bilioni zimeletwa mkoani Mbeya.
Kwa upande wake Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema pamoja na juhudi zinazofanywa katika kulinda na kutunza vyanzo vya maji, Wakala wa Misitu nchini (TFS) wamepanda miti katika utaratibu usio rafiki kwenye miradi ya maji ikiwamo Kiwira.
Amesema TFS wao wamekuwa wakilenga sana kuvuna miti kwa ajili ya biashara akibainisha kuwa kwa hali hiyo itaathiri malengo katika kunusuru mazingira haswa upatikanaji wa maji.
"Kuna miradi mikubwa ya maji inayoendelea lakini hawa TFS wao wanafikiria kufanya biashara zaidi kwa kupanda kwenye kingo za maji ili baadaye wavune kama kule Kiwira na mlima Mbeya, Kawetere na Rungwe" amesema Ackson
Mbunge huyo wa Mbeya mjini ameiomba serikali kukamilisha Sh250 bilioni ambazo zitakamilisha mradi wa maji wa Kiwira ambapo tayari Sh5 bilioni zimeshatolewa akieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo changamoto ya maji mkoani Mbeya itaisha.
"Mradi huu ni mkubwa sana na bajeti yake ni kubwa lakini tunashukuru tayari zimeletwa Sh 5 bilioni tunaomba serikali kazi itakapoanza kutekelezwa usikwame kwani kukamilika kwake tutaondokana na tatizo la maji mkoani Mbeya" amesema.
MWANANCHI