FikraPevu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2010
- 304
- 236
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha Sita yaliyofanyika Mei, 2014 mwaka huu, ambapo limesema ufaulu umeongezeka kwa jumla ya watahiniwa 30,225 sawa na asilimia 85.73 ambao wamefaulu katika madaraja ya I- III.
Akitangaza matokeo hayo leo Jumatano Julai 16, 2014 jijini Dar es salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dakta Charles Msonde, amesema kiwango cha ufaulu kwa mwaka huu kimeongezeka kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na kipindi cha miaka iliyopita.
Amesema Wavulana wameendelea kuongoza katika ufaulu wa jumla katika mtihani wa kidato Sita nchini, na kuwa kati ya watahiniwa waliofanya mtihani huo Wasichana waliofaulu ni 12,080 na wavulana waliofaulu ni 26,825.
Amesema jumla ya watahiniwa 41,968 walioandikishwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 12,674 (30.20%) na wavulana 29,294 (69.80%), watahiniwa wa shule walikuwa 35,650 ikilinganishwa na watahiniwa 43,231 walioandikishwa kufanya mtihani huo mwaka 2013.
Jedwali lifuatalo linaonesha ufaulu kwa kila daraja kwa watahiniwa wa shule
Soma Pia Matokeo mengine kuanzia 2009
| Daraja la Ufaulu | Wavulana | Wasichana | Jumla | |||
| Idadi | Asilimia | Idadi | Asilimia | Idadi | Asilimia | |
| I | 2,232 | 9.20 | 1,541 | 14.02 | 3,773 | 10.70 |
| II | 6,179 | 25.46 | 3,452 | 31.42 | 9,631 | 27.32 |
| III | 11,860 | 48.87 | 4,961 | 45.15 | 16,821 | 47.71 |
| IV | 3,474 | 14.31 | 946 | 8.61 | 4,420 | 12.54 |
| 0 | 524 | 2.16 | 88 | 0.80 | 612 | 1.74 |
''Kati ya watahiniwa 41,968 waliosajiliwa kufanya mtihani wa Kidato cha Sita Mei 2014, watahiniwa 40,695 sawa na asilimia 96.97 walifanya mtihani na watahiniwa 1,273 sawa na asilimia 3.03 hawakufanya mtihani na watahiniwa 35,650 waliosajiliwa, watahiniwa 35,418 sawa na asilimia 99.35 walifanya mtihani na kuwa wasichana walikuwa ni 11,022 (99.63%) na wavulana ni 24,396 (99.22%), watahiniwa 232 (0.65%) hawakufanya mtihani'' alikaririwa na FikraPevu.
Hata hivyo, amesema kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea 6,318 waliosajiliwa, watahiniwa 5,277 sawa na asilimia 83.52 walifanya mtihani na watahiniwa 1,041 sawa na asilimia 16.48 hawakufanya mtihani huo kwasababu mbalimbali.
Amebainisha kuwa ufaulu wa watahiniwa katika masomo yote (14) ya msingi umepanda ikilinganishwa na mwaka 2013 na kuwa ufaulu wa juu kabisa ni ule wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 99.88 ya watahiniwa waliofanya somo hilo wamefaulu.
Aidha, amesema ufaulu katika masomo ya Sayansi (Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati) umeendelea kuimarika kwa kulinganisha na ufaulu wa masomo hayo mwaka 2013.
Shule bora 10
Ametaja shule 10 zilizoongoza kitaifa kuwa ni Igowole ya Iringa, Feza Boys ya Dar es Salaam, Kisimiri ya mkoani Arusha, Iwawa ya Njombe, Kibaha ya mkoani na Marian Girls zote za mkoani Pwani, Nangwa ya mkoani Manyara, Uwata ya Mbeya, Kibondo ya mkoani kigoma na Kawawa iliyupo mkoani Iringa.
Shule 10 zilizofanya vibaya
Aidha, Msonde, ametaja shule ambazo zimefanya vibaya na kushika nafasi ya mwisho kuwa ni pamoja na...
Habari zaidi, soma=>Wavulana wapeta matokeo kidato cha Sita, 2014