SoC04 Wavuvi wawezeshwe kwa mikopo nafuu au Ruzuku, Ili kuboresha sekta hii

SoC04 Wavuvi wawezeshwe kwa mikopo nafuu au Ruzuku, Ili kuboresha sekta hii

Tanzania Tuitakayo competition threads

DALALI MKUU

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2022
Posts
2,011
Reaction score
4,705
Tanznaia Tuitakayo katika sekta ya UVUVI

UTANGULIZI

Tanzania tuitakayo kwa miaka miatano ijayo ni Kuona wavuvi wananufaika na Rasilimali za Uvuvi na zinabadilisha maisha yao kwa Ujumla.

Ifike hatua sasa wavuvi wakue wanufaike na Rasilimali hizo kwa kufungua masoko ya kimataifa, kuwa na njia bora za kuhifadhi na zana za kisasa za uvuvi.

Hivyo lazima kama taifa tuangalie namna bora na nzuri ya kufanya ili kufikia hatua hiyo.

SEKTA YA UVUVI NCHINI TANZANIA,

Sekta ya Uvuvi hapa nchini imekua na mchango mkubwa sana kwa taifa licha ya Changamoto Lukuki zinazoikumba sekta hiyo.

Serikali imekuwa ikichukua hatua kadhaa kuboresha na kuatatua chanagoto katika ekta ya uvuvi lakini bado haijawa na mchango mdogo sana katika kuchangia sekta hiyo Muhimu.

Katika mwaka 2020/2021, sekta imetoa ajira za moja kwa moja kwa wavuvi wapatao 194,804 na wakuzaji viumbe maji 31, 998 na zaidi ya Watanzania milioni 4.5 wameendelea kupata mahitaji yao ya kila siku kutokana na shughuli mbalimbali zikiwemo kuunda na kutengeneza boti, kushona nyavu, biashara ya samaki na mazao ya uvuvi pamoja na Baba na Mama lishe.

Pia, sekta ya uvuvi huchangia katika usalama wa chakula nchini ambapo samaki huchangia takriban asilimia 30 ya protini inayotokana na wanyama.

Pamoja na mchango Mkubwa bado sekta ya uvuvi inakabiliwa na chanagmo lukuki ikiwemo vifaa duni, masoko na hata uhifadhi.

kusaidia serikali ya Tanzania kuondokana na changamoto zinazowakabili wavuvi linaweza kujumuisha mbinu mbalimbali za kuboresha sekta ya uvuvi, uhifadhi wa rasilimali za baharini, na upatikanaji wa masoko. Hapa kuna baadhi ya maoni ya jinsi serikali inavyoweza kuchukua hatua:

KWANZA kabisa kwenye vifaa serikikali itoe Mikopo nafuu au ruzuku ili waweze kununua vifaa bora vya uvuvi pia kuanzissha Programu za ukarabati wa vifaa vya uvuvi, itasaidia kuleta ufanisi na ubora katika shughuli za uvuvi

1. KUBORESHA VIFAA VYA UVUVI:Serikali inaweza kuanzisha mipango ya kutoa mikopo au ruzuku kwa wavuvi ili waweze kununua vifaa bora vya uvuvi kama vile nyavu zenye ubora, boti za kisasa, au vifaa vya kuhifadhia samaki ili kuzuia uharibifu wa mazao.

2.ELIMU NA MAFUNZO: Serikali inaweza kuwekeza katika programu za elimu na mafunzo kwa wavuvi ili kuwajengea ujuzi zaidi kuhusu mbinu bora za uvuvi, uhifadhi wa mazingira ya bahari, na usimamizi wa rasilimali za baharini.Elimu hii ni pamoja na matumizi sahihi yateknoljia ya uvuvi (Fishing tecnlogy)

3.USIMAMIZI BORA WA UVUVI:Kuanzisha sera na sheria zinazolenga kusimamia uvuvi kwa njia endelevu na kuzuia uvuvi haramu au uvuvi usio na mipaka. Kupitia vyombo vya usimamizi kama vile mamlaka za uvuvi, serikali inaweza kusimamia na kudhibiti shughuli za uvuvi ili kuhakikisha kuwa rasilimali za baharini zinahifadhiwa kwa vizazi vijavyo.

4. KUWEZESHA MASOKO Serikali inaweza kushirikiana na sekta binafsi ili kuanzisha masoko ya uhakika kwa bidhaa za uvuvi. Hii inaweza kujumuisha kuanzisha minada ya samaki au kuwezesha upatikanaji wa teknolojia za kisasa za kuhifadhi na kusafirisha bidhaa za uvuvi kwenda masoko ya ndani na nje ya nchi.

5. KUHAMASIHA UTAFITI NA UBUNIFU:Serikali inaweza kuwekeza katika utafiti na maendeleo ili kukuza uvumbuzi katika sekta ya Hii inaweza kujumuisha kusaidia maabara za uvuvi, kuhamasisha uvumbuzi wa teknolojia mpya za uvuvi, au kusaidia kuanzisha miradi inayolenga kutatua matatizo maalum yanayowakabili wavuvi.

6.KUHAMASISHA UWEKEZAJI

Kwa kutekeleza hatua hizi na zingine zinazofanana, serikali ya Tanzania inaweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya uvuvi, kusaidia wavuvi kupata maisha bora, na kuhakikisha uhifadhi wa rasilimali za baharini kwa vizazi vijavyo.


MWISHO KWA KUMALIZIA


Vifaa bora, na masoko itavutia sana vijana wengi kuingia kwenye uvuvi hali amabyop itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa nchi yetu. Itavutia pia hata wasomi wa vyuo mbalimbali kufanya shughuli za uvuvi, uvuvi wenye tija

Pia sekta ya Uvuvi itafanikiwa kufikai malengo yake ya Kuchangia pato la taifa kwa asilimia 10% kama ilivyoainishwa kwenye hotuba ya bajeti ya Uvuvi na Ufugaji kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambayo sehemu ya hotuba hiyo ilieleza kwamba wizara hiyo imelenga hadi mwaka 2030 sekta ya uvuvi angalau iwe inachangaia 10% ya pato la Taifa.

Wizara ya uvuvi inatakiwa pia kushirikiana na kufanya akzi kwa ukaribu kabisa na wizara ya biashara na kuwa na maono ya pamoja ili kufanikisha sekta hii muhimu kwa uchumi wetu.
 
Upvote 3
Safi wazo zuri ila sijui kama serikali ipo sizriazi kwenye hiyo sekta
 
Ifike hatua sasa wavuvi wakue wanufaike na Rasilimali hizo kwa kufungua masoko ya kimataifa, kuwa na njia bora za kuhifadhi na zana za kisasa za uvuvi
Kwa kuwawezesha kutoa bidhaa bora tu ndio tutaweza kuwafikisha soko la kimataifa, twende kazi.

Vifaa bora, na masoko itavutia sana vijana wengi kuingia kwenye uvuvi hali amabyop itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa nchi yetu. Itavutia pia hata wasomi wa vyuo mbalimbali kufanya shughuli za uvuvi, uvuvi wenye tija
Ahsanye kwa kulimulika na hili👊
 
Back
Top Bottom