The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Baadhi ya wavuvi wanaofanya shughuli zao ndani ya Ziwa Victoria wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti wimbi la uvamizi linalodaiwa kufanywa na maharamia wanaodaiwa kutoka nchi jirani.
Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evance Mtambi baadhi ya wavuvi hao wamesema uvamizi kwa sasa umerejea kwa kasi ambapo wananyang'anywa samaki pamoja na mashine na wapokataa wanajeruhiwa kwa kupigwa.
Charles shishi nimiongoni mwa wavuvi ambao wamekutana na kadhia hiyo ambapo alisema pamoja na uwepo wa Askari Wanamaji lakini wamebaini baadhi yao wamekuwa wakishiriki kunyang'anya samaki kutoka kwa wavuvi wakenya hali wanayoamini inachagiza na wao kukutana na matukio hayo.
"Mkuu wa mkoa tunatoa taarifa kwa polisi wanamaji chakushangaza mnawaonesha wale pale lakini wakifika wanaongea hawa wanapita huku na hawa wanapita huku hampati mwafaka nini kimeamuliwa tunappteza mali zetu na hawatusaidiia "Alisema Charles
Baada ya kusikiliza malalamiko hayo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Rorya Dkt. Khalfan Haule kukaa na kamati ya Usalama katika Wilaya hiyo na kuwashirikisha wavuvi kuyabaini maeneo wanayovamiwa kisha hatua zaidi kuchukuliwa ili kuhakikisha wavuvi wanakuwa Salama.
Katika hatua nyingine Kanali Mtambi amemtaka Mkuu huyo wa wilaya kukaa na viongozi wa upande wa nchi jirani ili kuwaeleza juu ya uwepo wa matukio hayo na kushirikiana nao katika kuweka hali ya usalama kwa wavuvi wote na kukomesha vitendo vya uhalifu.