Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mhe. Kitandula ameyabainisha hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe Josephat Sinkamba Kandege (Mb) aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani mahsusi wa kuhakikisha Maporomoko ya Kalambo yanatangazwa kitalii.
Aidha, Mhe. Kitandula aliongeza kuwa Serikali imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuendeleza na kuyatangaza maporomoko ya Kalambo ikiwemo kuboresha miundombinu mbalimbali kwenye hifadhi ya mazingira asilia ya Kalambo na kufanya kampeni za kuyatangaza maporomoko hayo.
Soma Pia: Bodi ya utalii tanzania kuendelea kuutangaza mlima meru
Aidha Mhe. Kitandula alitanabaisha kuwa katika uboreshaji wa miundombinu, Serikali imeboresha barabara; njia za waenda kwa miguu; ngazi za kushuka kwenye maporomoko na kupandisha; miundombinu ya vyoo; mabanda ya kupumzika wageni na eneo la maegesho.
Vilevile serikali imefanya matangazo kwa kutoa makala maalum na kurushwa kwenye televishen lakini pia kumekuwa na uandaaji wa matukio na vifurushi vya misimu maalum ikiwemo kuandaa mabango na vipeperushi na kutumia njia za kidijitali katika kutangaza maporomoko hayo.
Maporomoko ya Maji Kalambo, ni kivutio muhimu cha utalii nchini na barani Afrika kwa ujumla. Maporomoko haya yana urefu wa mita 235 ambao unayafanya kuwa ya kwanza kwa urefu nchini Tanzania na ya pili Barani Afrika baada ya Maporomoko ya Maji ya Victoria