Uswahili ni kwetu kuna wawekezaji kutoka china.
Jamaa ni balaa wanaharibu miundo mbinu ya kimasikini tuliyo nayo ile mbaya kwani wanapitisha yale maroli yanayobeba macointainer bila huruma na kusababisha barabara kudidimia na kuwa kisiwa kila baada ya nvua kunyesha.
Wanamtaa wote hatuoni faida ya hawa wawekezaji kabisa zaidi wanaleta machungu kwa sisi tunaotumia barabara hiyo.
Serikali inapaswa kuangalia haya mamabo ya wawekezaji kujiamulia mambo mengine yanayo kera raia na kuharibu miundo mbinu yetu
hakuna serikali ya mtaa hapo kwenu?? hakuna wajumbe wa shina?? wanafanya kazi gani??? anzia huko
Ni malori mangapi kwa wastani yanayoendeshwa na wachina, na mangapi yanayoendeshwa na wasio wachina (ambao pengine nao si watanzania, ila ni weusi)?
Isije ikawa kama magazeti ya shigongo ambaye akiona machinga wa kichina watano, anasema wachina wamejaa. Lakini kukiwa na wasomali au wakenya 20, hamna kinachosemwa!