wawekezaji wa uchimbaji wa madini Lushoto magamba madini

wawekezaji wa uchimbaji wa madini Lushoto magamba madini

samilakadunda

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2011
Posts
1,780
Reaction score
355
serikari ya muh kikwete mwatupeleka wapi?wkwanini mnatutesa sisi wananchi? kwafaida yenu ninyi na familia zenu? kwanini tunaleta shughuri ambazo hakika athari zake nikubwa kuliko faida? ninani anayepata faida juu ya hawa wawekezaji? hatutakubali kamwe kutuingiza katika matatizo haya kwakuwaneemesha walio wachache, napenda kusema tumechoka nahatutakubali uchimbaji huu kufanywa katika maeneohaya wilaya ya Lushoto vijiji vya magamba.
 
Mjumbe kabla hatujasikia ni kina nani tunao wakatalia kuwekeza katika mradi huu ni vyema tungefanya uchunguzi wa kina kujua faida ya mradi huu kwa mji wa lushoto na Taifa mmi sikuungi mkono kwa ushawishi wako ya kuwa hatutaki mradi wewe sema hutaki usitujumlishe sisi sote maana sisi vijana wa magamba tumekuwa hatuna kazi za kudumu takribani miaka kumi sasa na tumeishawahi kusikia habari ya mradi wa aina hii lakini kwa sababu ya kikundi cha watu wachache na wasiopenda maendeleo ya magamba na vijana wa Magamba waliuzuia mradi huo kwa kisingizio kuwa tutakufa madini haya yanasumu,lakini MUNGU katusikia tena katupa mradi huu tena ambao umekuja na watanzania wenzetu wametuelezea na tumeridhika na utaratibu wao hivyo sisi tunaunga mkono mradi bila kukubali wa ushawishi wa mtu au watu wanaotaka wao peke yao wawe na pesa na kututumia sisi kama vibaraka wao wa kuwaweka madarakani tuanajua mchezo wote mchafu unaopangwa na kundi hilo la wasiotaka maendeleo yetu kwa kuwashawishi wanachuo wa sekomu kutotuunga mkono katika kazi hii.
Mjumbe napenda na sisi tukufahamishe kuwa huyo anaye washawishi bila kukupa nafasi ya kumuuliza swali juu ya hasara za mradi na faida zake anakimbilia kukushawishi uende mkutanoni ukapinge jumamosi kupinga mradi anataka kukutumia ili kufikisha malengo yake na wewe ukiwa kama msomi na mtu mwenye uelewa unaingia kwenye mtandao ambao unatusaidia kujadili hoja za msingi bila uchunguzi wa kina unapinga mradi jaribu kufikiri usikubali kutumiwa na wanasiasa wachache wanaotaka lushoto ikae juu ya Aluminium na wananchi wake waendelee kuomba omba huku uchumi wameukalia Muda ni huu sasa kijana wa lushoto kujitokeza ili kupiga kura yako ya ndio maana wamiliki wa uwekezaji huu ni watanzania wenzio kilio cha watu wengi wa tanzania kuwa leseni za uchimbaji zipewew wazawa.
Rai yangu kwa wadau wa jamii forum mtusaidie kutupa ufafanuzi juu ya faida ya uchimbaji wa bauxite na hasara zake na kama bauxite inasumu ndani yake kwa maisha ya watu,tunahitaji kesho kwenda kutoa maoni yetu juu ya namna gani uchimbaji huu utafanyika katika eneo la magamba na sisi ni vijana wagamba tunahitaji ajira tumechoka na maisha ya ngoja kesho ngoja kesho.
 
Hizi faida ambazo zitakuja na mradi huuni pamoja na

AJIRA hii ni kwa vijana kwa mujibu wa wawekezaji hawa wa boxite lushoto magamba wameahidi nafasi za kazi kwa vijana 100 mara tu mradi huu utakapoanza.

Kwa mujibu wa wawekezaji hawa biashara hii itakuwa ni ya kimataifa hivyo Tanzania itaongeza akiba yake ya pesa za kigeni jamabo ambalo liainua uchumi wa nchi.

kwa mujibu wa wekezaji hawa bauxite itauzwa China na India hivyo itasafirishwa kupitia bandari ya Tanga hii ni fursa kwa Mamlaka ya bandari tanga kuongeza kipato na kuanza kuchangia katika pato la nchi kama zamani tanga ilipokuwa ikisifika kwa viwanda ambavyo vingi wakati huu vimefungwa,biashara hii ya bauxite lushoto itaiingiza bandari ya TANGA katika ramani ya dunia tena baada ya muda mrefu kufunikwa na bandari ya mombasa ambayo kwa wakati huu ndiyo inatumika kupitisha mizigo mingi toka nje.

Kwa mujibu wa wawekezaji wanasema watajenga yard kubwa Mombo ambayo itatumika kama eneo la kukusanyia mzigo huu na kisha kusafirihwa kwenda tanga kazi ya usafirishwaji wa bauxite itafanywa na magri ya watanzania wenzetu huu ni mchango kwa uchumi wetu sote tusiangalie kazi hii kisiasa sana kwa kuwaambia viongozi wamepewa pesa ,ila tuiangalie kuwa sasa watanzania wameanza kuamka na kumiliki lasilimali zao wenyewe.

Nawaomba wajumbe tuwaunge mkono watanzania wenzetu wajasiliamali wadogo katika harakati hii ya kuanza safari ya uuzaji wa madini ya viwandani na watanzania wakiwa ndio wamiliki wa machimbo haya kwa nchi za nje .kesho tukajitokeze magamba kwenye mkutano tukasikilize wawekezaji wetu wa kitanzania watasema nni kilicho tofauti na wamiliki wengine wa kigeni wano miliki migodi hapa nchini.
 
Ni sera ya Tanzania Kuvutia uwekeazji wa ndani na wa nje, Tanzania imejaliwa rasilimali nyingi za asili ikiwemo Madini. Kwa bahati mbaya Watanzania wengi tunafahamu madini ya vito kuliko ya viwanda. Mradi huu ni wa maana kwani utaongeza pato la taifa, utaoongeza ajira, na utahamasisha maendeleo kwani Eneo la mradi na maeneo jirani yote yatanufaika.

Watanzania tuache woga, Nchi yetu inaongozwa kwa sheria kanuni na taratibu kwa kila jambo. Si kila uchimbaji wa madini ni mbaya , au ni ufisadi au ni hatari ndo maana tuna mamlaka zilizowekwa kisheria kufanya kazi ya kupembua madahara na faida za kitu chochote katika jamii yetu kabla ya kuanza.

Mradi huu unamilikiwa na watanzania, wachimbaji wadogwadogo ambao wamepewa leseni kwa mujibu wa sheria, na wametafuta wabia watakaofanya nao mradi huu, sawasawa na sera ya serikali ya kuhamasisha ubia kibiashara kati ya serikari na watu/taasisi binafsi.

Kesho ni siku ya mkutano tujitokeze kwa wingi kuunga mkono mradi ili tuanze kunufaika na uuzaji wa madini haya nje ya nchi. Tuwapinge wote wanaoleta siasa kwenye mambo yanayohusu maisha yetu. Magamba oyeeee.
 
Nikweli wajumbe mliochangia ujumbe huu mposahihi kwa mawazo yenu, tusichukulie swala hili kishabiki wala kimaslahi ya watu wachache, hebutuchukue japo dakika 10kutafakari juu ya shughuri mbalimbali za madini zinazoendelea hapa Tanzania, je kunafaida gani wanazozipata wananchi maskini wanaoyazunguka maeneo hayo? Mfano machimbo ya buwagi, mwadui wanaenchi wamenufaika nini? Nakumbuka vijana kwa wazee walivokuwa wakishangilia Rais Obama alipokuwa akigombea uraisi Marekani wakiamini wataneemeka na ushindi wake, ameshinda kawaulize kawafanyia nini??. Naomba kuchukuafrusa hii kumaomba hao wawekezaji na serikari kwa ujumla watoelimu pamoja na asasi zisizo za kiserikari juu ya faida na hasara za uwekezaji huu, namkumbuka mwalimu Julias Nyerere aliesema madini hayaozi hivo hatunabudi kujiandaa na kuelimika juu ya madini hayo ili tuweze kufaidi sisi wananchi na sio wajanjawanja wa wachache.
 
Back
Top Bottom