Wawekezaji wa UTT AMIS pitia hapa

MONA WA KYEN

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2016
Posts
340
Reaction score
271
Natumaini mko buheri wa afya kabisa.

Kila wakati nikiwa naangalia taarifa ya bahari ya ITV huwa naona taarifa ya mifuko ya UTT AMIS na nimekuwa sielewi kwa hakika ni nini hasa.

Mwenye maelezo ya kutosha kuhusu hii mifuko naomba anisaidie maelezo yake na
1. Mtu anawezaje kunufaika na kuwekeza huko?
2. Faida yake ikoje, ufanisi wake n.k

Ahsanteni karibuni wataalamu

------------

Nani anaruhusiwa kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na UTT?

Mifuko hii ni kwa ajili ya watanzania wanaoishi nchini na nje ya nchi.Wanaweza wakajiunga mtu mmoja mmoja au kwa pamoja (jointly), wazazi kuwawekezea watoto wao, vikundi mbalimbali vya kijamii, NGOs, taasisi mbalimbali, mifuko ya hifadhi za jamii, mashirika ya umma, Banks n.k

Nawezaje kujiunga na mifuko unayoendeshwa na UTT-AMIS?
Ni rahisi.Tembelea Bank mbalimbali. Unapaswa kuwa na kitambulisho kama vile Kitambulisho cha mpiga kura , Kitambulisho cha utaifa, Pasipoti, leseni ya kuendesha gari, au kitambulisho cha kazi. Baada ya kujaza fomu akaunti ya mfuko maalum itafunguliwana utaweza kuanza kuwekeza.

Je kuna kiwango cha chini cha kuanza kuwekeza ?
Kima cha chini cha uwekezaji wa awali kimeelezwa katika waraka wa Toleo (Offer Document)katika mfuko husika. Mifuko ina viwango tofauti vya kuanza kuwekeza. Uwekezaji wa awali unaweza fanyika kwa kima cha chini kabisa cha Tsh 5,000 Mfuko wa Umoja, Tsh 8,340 kwa mwezi kwa Mfuko wa Wekeza Maisha na Tsh.10,000 kwa Mfuko wa Watoto, Tsh. 15,000 mfuko wa Kujikimu na Tsh. 5,000,000 kwa mfuko wa Ukwasi.

Je,ninatakiwa kuongeza uwekezaji wangu kila mwezi?
Haikulazimu kuongeza uwekezaji wako kila mwezi. Kuna njia mbili kuwekeza katika Mifuko ya uwekezaji wa pamoja. Kwanza, mkupuo ambapo kuwekeza kiasi mara moja na hakuna uwekezaji wa ziada baada ya hapo. Pili, kuweka kwa mara kwa mara, ambapo kuwekeza kiasi awali, kisha kuendelea na uwekezaji wakati wowote unapopata fedha.

Je, faida ipatikanayo katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni ya uhakika?
Faida itategemea ufanisi wa uwekezaji yaliyofanywa na Meneja wa Mfuko na pia hutegemea hali ya uchumi na masoko ya fedha.

Ninatakiwa kuwekeza katika mifuko kwa muda gani?

Kwa kawaida, wawekezaji wanashauriwa kuwekeza kwa muda muda mrefu . Mifuko ya uwekezaji inaweza kuwa kwa ajili ya uwekezaji wa muda wa kati au muda mrefu.Inashauriwa kuendelea kuwekeza katika mifuko kwa muda mrefu ili kupata mapato bora zaidi.

Je, ninaweza kuuza vipande vyangu wakati wowote?

Ndiyo, unaweza kuuza vipande wakati wowote kama ilivyo ainishwa katika waraka wa toleo wa mfuko husika. Isipokuwa Mfuko wa Wekeza Maisha,mwekezaji anaruhusiwa kuanza kuuza baadhi ya sehemu ya uwekezaji wake baada ya miaka mitano ya uwekezaji.

Je, ninahitajika kulipa kodi wakati ninapo uza vipande vyangu?

Hapana, hutakiwi kulipa kodi unapouza vipande vyako au unapopata gawio.Meneja wa mfuko analazimika kulipa gharama zote za uendeshaji ikiwepo na kodi.Hivyo thamani halisi ya kipande.

Ninawezaje kujua ninapata faida au hasara?

Meneja mwendeshaji wa mfuko analazimika kutoa thamani halisi ya kipande kila siku ya kazi. Jinsi rasilimali za mfuko zinavyoongezeka ndivyo thamani ya kipande inavyoongezeka. Na kwa upande mwingine na jinsi rasilimali za mfuko zinapungua pia thamani ya kipande ndivyo inavyopungua hivyo kuashiria hasara kwa mwekezaji.Mwekezaji anaweza kufuatilia thamani halisi ya kipande kila siku za kazi kupitia magazeti ya Mwananchi,Daily News na The Guardian.

Je, mwekezaji anaweza kuteua mrithi wa uwekezaji wake iwapo atafariki?

Ndiyo. Uteuzi unaweza kufanywa wakati wa kujaza fomu ya kujiunga. Na iwapo mteule atakuwa ni mtoto chini ya umri wa miaka 18 basi mzazi anatakiwa kuteua mwangalizi ambaye ana umri zaidi ya miaka 18

Ninahitajika kufanya nini baada ya kuwekeza?

Baada ya wiki 2-3 za kuwekeza , utapokea taarifa ya akaunti yako ya uwekezaji kutoka UTT. Angalia juu ya taarifa na kuhakikisha taarifa na miamala yote katika taarifa ni sahihi.

Pia unaweza kufuatilia mwenendo wa uwekezaji wako kupitia matoleo ya bei halisi za thamani ya mifuko katika magazeti na wovuti.

Pia wawekezaji wenye uwezo wa kushiriki mkutano wa mwaka wanashauriwa kushiriki ili kuweza kupata taarifa za utendaji wa mifuko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…