The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti ameuagiza Uongozi wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kuwaandikia notisi ya kuwatoa kwenye vitalu wawekezaji waliokiuka masharti ya Mkataba wa kukodisha mashamba katika Ranchi ya Usangu.
Mnyeti ametoa maelekezo hayo Machi 7, 2025 Wilayani Mbeya wakati wa Ziara yake Kwenye Ranchi ya Usangu ambapo amesema serikali imetoa mashamba hayo kwaajili kuzalishia mifugo na sio shughuli za Kilimo.
” Mashamba haya ni ya kwaajili ya Mifugo lakini kuna watu walikuja kutaka kukodisha kwaajili ya kuzalisha mifugo lakini wamegeuza matumizi na sasa wanalima hili halikubaliki, Nawapa siku tatu Narco kuwaandikia notisi wote waliokiuka”alisema Mhe. Mnyeti.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) Bw. Mrida Mshota amesema ili kuweza kunufaika na sekta ya mifugo lazima jamii ya wafugaji na wawekezaji kukubaliana na mabadiliko.