Hapo jana, katika eneo alipouliwa Generali Chirimwami, lililokuwa mikononi mwa SAMIRDC na MONUSCO, M23 iliwafukuza na kuwasogeza nyuma. Kundi la FDLR chini ya uongozi wa General OMEGA, na lenyewe lililokuwa chini ya mlima Nyiragongo, na lenyewe limezingilwa na kuachiwa tu njia ya kutokea. Lakini, njia ya kutokea na yenyewe inaelekea Kibumba, ambayo ni makazi ya M23. Taarifa za chini chini, ni kwamba Mzelendo au FARDC atakaekamatwa au kujisalimisha, atapokelewa na kulindwa na M23. Mrundi, Mtanzania na raia wengine, watakamatwa kama wafungwa wa vita, na badae watarudishwa kwao. Lakini FDLR, akikamatwa, yeye ni kifo tu. inasemekana Omega tayari ameshakimbizwa Kinshasa.
Kwa sasa, jeshi la Tanzania ndo inasemekana linafanya maandalizi ya kukabiliana na kundi hilo. Lakini ukiangalia uhalisia wa vita hivi, walichoshindwa wengine, JWTZ haileti matumaini. Baada ya MONUSCO na SAMIDRC kuwasubilia eneo la tukio, walishitukia makombola yanarushwa kwao kutokea upande wa nyuma, ambapo kwa sasa wanajeshi 9 wa upande huo ndo wameripotiwa kujeruhiwa.