Wazalendo tusaidiane kuishauri Wizara ya Maliasili na Utalii kuboresha utalii

Wazalendo tusaidiane kuishauri Wizara ya Maliasili na Utalii kuboresha utalii

falcon mombasa

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
9,189
Reaction score
9,299
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Mimi sio mtaalamu sana wa masuala haya ila naamini bado sio sababu ya kushindwa kukusanya maoni kuishauri serikali kupitia wizara ya utalii nini kifanyike kukuza utalii.

Nasisitiza tuweke uzalendo kwanza kwenye thread hii. Hii ni nchi yetu sote sisi na vizazi vijavyo vinahaki kufurahia maliasili zilizopo nchini.

Wizara ya utalii kupitia mh waziri Kigwangala wanafanya kazi kubwa kuhakikisha tunajitangaza.

Lakini kusema ukweli kasi ya watalii wanaoingia nchini kulinganishi na rasilimali zilizopo ni ndogo sana sawa na hakuna.

Hebu vuta picha mji wa New York peke yake kwa mwaka unapokea watalii milion 67. Huku kile kieneo
cha central park pekee alipo shoot diamond wimbo wake wa baila kinapokea watalii 25 million

Tukirudi kwetu sisi takwimu zinaonyesha tunapokea watalii milion na nusu, 150,0000 idadi hii ni ndogo sana lazima tuamke yaani mbuga ya Serengeti pamoja nakuwa kwenye rekodi za dunia lakini inapokea watalii wasiozidi laki tano.

Wazalendo lazima tuamke tuishauri serikali kipi cha kufanya.

Kama nilivyosema mwanzo mimi sio mtaalamu sana wa mambo haya ila nitapigania nchi yangu.

Serikali lazima ikubali kuingia gharama kubwa kujitangaza ni heri tukakubali kupata hasara mwaka mzima lakini tuwe tumejitangaza kwa miaka 1000 ijayo.

Serikali na mh Kigwangala ni ukweli usipingika watalii wengi nchini wanatokea Marekani. Sasa basi unaonaje Kama tutatumia gharama kwa mchanganuo ufuatao japo sijui Kama unawezekana au lah ila ni sehem ya ushauri tu

Tafuta macelebrity wakubwa marekani wa kutoka kila sekta watimie hamsini

Hawa ongea nao vizuri waorganize waje huku
Tunawatumia dege let moja Boeing liwafuate kwa gharama zetu sisi waje bongo

Wahakikishiwe usalama wait na mali zao maana katika kitu tutajenga au kubomoa endapo usalama wao unakuwa hafifu .pia tuhakikishe wahudumu wetu ni waaminifu jamani yaani tunatia aibu wahudumu wetu kudokoa vitu vya wageni aibu kubwa na hawa wadokozi wapewe adhabu kali kama wahujumu wa taifa.

Hawa macelebrity baada ya kutua bongo kwa gharama zetu tuwachukue hadi kwenye hotel zetu kwa gharama zetu waende kutembelea vivutio vyetu kwa gharama zetu bureeeee tusiwachaji hata mia na tuwape vip treatment (USISEME haiwezekani sema inawezekana)

Wakae bongo hata wiki nzima kisha tuingie nao mkataba kuwalipa kwa mwaka hata mmoja yaani kwa kila mapato yatokanayo na utalii Basi nao wanamgao wao asilimia fulani.

Pia kuna kitu kimoja au viwili vitatu vinawakera Sana watalii

Sisi watanzania tunatabia kuwaona watalii Kama walking ATM MACHINE tunatia aibu na hiki kitu kinawafanya wasiwe comfortable.

Pia sisi watanzania tunatabia ya kuwaita watalii wazungu hakuna neno linawafanya wajisikie vibaya kama wakijua tafsiri ya neno mzungu.wengi wanasema ni indicator of racism.

Mwisho tuna wale wauzaji bidhaa mbali mbali kwa watalii hawa ndugu zetu wanatabia ya kumzonga mtalii hata Kama mtalii alisema hanunui hiko kitu wao wanatabia ya kuwabembeleza hadi wanaboa.

Umemtangazia mtalii bidhaa yako akakwambia thank you yanini uendelee kumbembeleza hadi anakereka.

Pia wageni wetu haswa watu wa magharib wanautamadun wao na moja ya vitu ambavyo ni utamaduni wa ajabu ni ushoga
Tafadhali hata Kama kwetu ushoga ni kosa basi tusiwatreat vibaya hawa watu kiasi ambacho watarudi kwao na image mbaya kuhusu Tanzania yaani tujaribu hata kuigiza Kama hatuna neno nao ili wasijisikie unsafe being in Tanzania.

Je, wewe unashauri nini kifanyike kukuza utalii angalau kufikia utalii wa central park tu kabla hatujafikia utalii wa New York nzima.
 
pia tuhakikishe wahudumu wetu ni waaminifu jamani yaani tunatia aibu wahudumu wetu kudokoa vitu vya wageni aibu kubwa na hawa wadokozi wapewe adhabu kali kama wahujumu wa taifa

Udokozi mara nyingi hutokea pale mtu anapokuwa hajaridhika na anacholipwa.
Malipo ya hawa wahudumu sio mazuri, wengi wanaponea kwenye tips.
Unakuta mtu anaweza kukusanya tips za wiki moja ...zikazidi mshahara wake wa mwezi...sasa siku akizikosa ...lazima atadokoa..maana mshahara haukidhi mahitaji yake.

Tunajua mbunga ziko chini ya Serikali...tunasahau ewendeshaji wake uko chini ya watu binafsi(baadhi). Katika kupanga Bei na kuzitangaza nyingi zinategemeana na mmiliki wa Camp husika. Serikali ikae nao ndio wakubaliane jinsi gani watasaidiana kutangaza Bisahara yao.

Tudumishe utalii wa ndani pia...itasaidia kujitangaza nje bila kuitegemea serikali na kwa gharama nafuu.
 
Wanaye Prof Wineaster Anderson mwenye taaluma ya marketing of tourism services kwenye bodi yao... Watumie ushauri wake.
 
Tanzania itaendelea pale Siasa ikijua mipaka Yake. Uchawi wa hii nchi Ni siasa na wanasiasa kujiona Ni wataalamu wa kila kitu.

Kwa akili yako unadhani hayo uliyoandika pale Tourism Board au Tanapa hawajui ?? Au unadhani TaToA hawajui?? Hawa ndio wataalamu wa haya Mambo wanajua fika ila kwasababu nchi hii mwanasiasa ndio kila kitu huoni wakipewa hata space ya kufanyia kazi utaalamu wao, matokeo Yake mwanasiasa anafanya vile anavyoona inafaa kumbe ndio anaipoteza sector ya utalii.

Kipindi Cha kikwete Tanapa na Board ya utalii walikuwa wanapeleka matangazo mpaka kwenye ligi kuu ya uingereza hususani kwenye team ya Sunderland na Stock city. Awamu hii wataalamu hawapew nafasi kabisa lazima utalii ushuke.

Kingine uchawi mkubwa wa Tanzania huwa tunadhani nchi yetu ndio yenye vivutuo vingi kwahyo lazima watakuja tu haina haja ya kufanya lolote.. Utalii sio kuwa na masimba tu. Kuna nchi hazina wanyama Kama Tanzania na zinapokea watalii wengi wa Beach tourism zaidi ya TANZANIA. Tubadili hizo mindset.

IMG_1om394.jpeg
 
Udokozi mara nyingi hutokea pale mtu anapokuwa hajaridhika na anacholipwa.
Malipo ya hawa wahudumu sio mazuri, wengi wanaponea kwenye tips.
Unakuta mtu anaweza kukusanya tips za wiki moja ...zikazidi mshahara wake wa mwezi...sasa siku akizikosa ...lazima atadokoa..maana mshahara haukidhi mahitaji yake.

Tunajua mbunga ziko chini ya Serikali...tunasahau ewendeshaji wake uko chini ya watu binafsi(baadhi). Katika kupanga Bei na kuzitangaza nyingi zinategemeana na mmiliki wa Camp husika. Serikali ikae nao ndio wakubaliane jinsi gani watasaidiana kutangaza Bisahara yao.

Tudumishe utalii wa ndani pia...itasaidia kujitangaza nje bila kuitegemea serikali na kwa gharama nafuu.
Utalii wa ndani ? Hivi unayajua maisha ya watanzania mkuu ??

Unadhani Tanznaia Ni Dar es salaam tu ... Kuna Jamii Tanzania mlo mmoja tu ni shida ndio aende kutalii [emoji3].

Utalii wa Tanzania mapato yanatokana na Foreigners ndio maana unaona Arusha iko kimya kwasasa.

Kutegemea utalii wa ndani utoe mapato ni sawa na kutegemea Bikra katika wodi za wajawazito.
 
Udokozi mara nyingi hutokea pale mtu anapokuwa hajaridhika na anacholipwa.
Malipo ya hawa wahudumu sio mazuri, wengi wanaponea kwenye tips.
Unakuta mtu anaweza kukusanya tips za wiki moja ...zikazidi mshahara wake wa mwezi...sasa siku akizikosa ...lazima atadokoa..maana mshahara haukidhi mahitaji yake.

Tunajua mbunga ziko chini ya Serikali...tunasahau ewendeshaji wake uko chini ya watu binafsi(baadhi). Katika kupanga Bei na kuzitangaza nyingi zinategemeana na mmiliki wa Camp husika. Serikali ikae nao ndio wakubaliane jinsi gani watasaidiana kutangaza Bisahara yao.

Tudumishe utalii wa ndani pia...itasaidia kujitangaza nje bila kuitegemea serikali na kwa gharama nafuu.
Hakika umezungumza mazuri sana lakin watanzania wengi wanaonekana hawana muamko na utalii wa ndani
 
Tanzania itaendelea pale Siasa ikijua mipaka Yake. Uchawi wa hii nchi Ni siasa na wanasiasa kujiona Ni wataalamu wa kila kitu.

Kwa akili yako unadhani hayo uliyoandika pale Tourism Board au Tanapa hawajui ?? Au unadhani TaToA hawajui?? Hawa ndio wataalamu wa haya Mambo wanajua fika ila kwasababu nchi hii mwanasiasa ndio kila kitu huoni wakipewa hata space ya kufanyia kazi utaalamu wao, matokeo Yake mwanasiasa anafanya vile anavyoona inafaa kumbe ndio anaipoteza sector ya utalii.

Kipindi Cha kikwete Tanapa na Board ya utalii walikuwa wanapeleka matangazo mpaka kwenye ligi kuu ya uingereza hususani kwenye team ya Sunderland na Stock city. Awamu hii wataalamu hawapew nafasi kabisa lazima utalii ushuke.

Kingine uchawi mkubwa wa Tanzania huwa tunadhani nchi yetu ndio yenye vivutuo vingi kwahyo lazima watakuja tu haina haja ya kufanya lolote.. Utalii sio kuwa na masimba tu. Kuna nchi hazina wanyama Kama Tanzania na zinapokea watalii wengi wa Beach tourism zaidi ya TANZANIA. Tubadili hizo mindset.

View attachment 1472902
Siasa imekuwa kikwazo kikubwa kwa awamu hii kila kitu kinafanyika kisiasa ...hatujui watoto wetu watarithi nini toka kwetu
 
Hakika umezungumza mazuri sana lakin watanzania wengi wanaonekana hawana muamko na utalii wa ndani
Muamko utoke wapi kama hatujitangazi?
Najua kiingilio cha Mzawa nitofauti na mgeni.

Je malipo ya kutalii na kulala mbugani yanatofauti kati ya mzawa na mgeni?(tuanzie hapo)

Muamko unatakiwa uwazie tokea utotoni...ndio sasa unaona shule zinapeleka watoto mbugani...ila kwa wale wenye uwezo.

Sehemu nyingi za kitalii kwenye mataifa mengine....bei zao ni sawa kwa wageni na wazawa(nilizopitia), hii inawezesha utalii wa ndani kuwa mrahisi sana.
 
Hili la Bei za hotelin uko sahihi sana ziko juu mno halafu kibaya zaidi ukienda wewe mwenyeji utapewa tour guide wanaojifunza akienda mgeni anapewa senior tour guide
 
Back
Top Bottom