Wazalendo waasisi 17 wa tanu nani anaewakumbuka leo siku ya saba saba?

Wazalendo waasisi 17 wa tanu nani anaewakumbuka leo siku ya saba saba?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
1148333

Picha ya Waasisi wa TANU
7 Julai, 1954

Leo ni Saba Saba siku ambayo tarehe 7 Julai 1954 wazalendo 17 walikutana katika ofisi ya TAA New Street kuasisi chama cha TANU, chama ilichokuja kudai uhuru wa Tanganyika. Si wengi wanaojua historia ya wazalendo waasisi hawa.

Leo nimeingia Maktaba kuwatafuta hawa wazalendo waasisi wa TANU ili tuwaadhimishe.

Katika uasisi wa TANU Jimbo la Mashariki ndilo lilikuwa na wajumbe wengi kushinda yote liliwakilishwa na, ndugu wawili Abulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, Tewa Said Tewa, Patrick Kunambi, Kasella Bantu, John Rupia, Julius Nyerere na C. O. Milinga.

Hawa ni wajumbe tisa na takriban wote wanafahamika angalau kwa majina yao kutajwa ila Milinga.

Sijakutana na mtu anaemfahamu Milinga alikuwa nani, kafanya nini na nini historia ya maisha yake.

Jimbo la Kaskazini liliwakilishwa na Joseph Kimalando na Japhet Kirilo; Jimbo la Ziwa liliwakilishwa na Abubakar Kilanga, L. M. Makaranga na Saadan Abdu Landoro.

Jimbo la Kaskazini alikuja Japhet Kirilo na Jimbo la Magharibi liliwakilishwa na Germano Pacha.
Nani hii leo siku ya saba saba anawajua au kuwakumbuka wazalendo waasisi hawa wa TANU?

Katika hawa wazalendo ni mmoja tu Saadan Abdu Kandoro ndiye aliyenyanyua kalamu kuandika historia ya TANU – ’’Mwito wa Uhuru.’’

Wengine katika kundi lile la wazalendo waasisi waliandika ingawa si kitabu kuhusu historia ya TANU ni Joseph Kasella Bantu na Lameck Bugohe ambao wao wameandika makala.

Jambo la kusikitisha ni kuwa hawa wote wanalalamika kuwa historia ya TANU haijaandikwa.

Kasella Bantu amekuwapo katika harakati na mipango ya kuunda TANU toka siku ya kwanza kwani yeye mwaka wa 1952 ndiye aliyempeleka Julius Nyerere nyumbani kwa kwa Abdul Sykes na pia alikuwapo na kushiriki katika uchaguzi wa mwaka 1953 uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo ambao Nyerere alipochaguliwa kuwa rais wa TAA baada ya kumshinda Abdul Sykes.

Kasella Bantu hana asilojua katika historia ya TANU.

Kasella Bantu alipoandika alieleza mchango wake binafsi katika TAA na TANU.

Lameck Bugohe alikwenda mbali zaidi yeye alisema alikuwa na nia ya kuasisi chama cha siasa kupigania uhuru wa Tanganyika kwa hiyo haikuwa ajabu yeye kuwa mmoja wa wazalendo waasisi wa TANU.

Kabla ya kufariki mwaka wa 2015 Bugohe alipata kuandika makala akilalamika kwa kupuuzwa kwa historia ya waasisi wa TANU.

Miaka mitano baadae Lameck Bugohe akafariki dunia na kuzikwa kimya kimya kama vile hakuwa na mchango wowote katika historia ya Tanganyika.

Hakupata mazishi yanayomstahiki mzalendo aliyepigania uhuru na kuwa mmoja wa wazalendo 17 walioasisi TANU mwaka 1954.

Kasella Bantu amekufa hakuna aliyekuwa na habari na yeye na hii ndiyo historia ya hao waasisi wote.

Ukiona muasisi kapata mazishi makubwa basi si kwa ajili ya mchango wake kwa taifa bali kwa umaarufu wake mwenyewe binafsi.

Haya yameonekana katika maziko ya Abdul Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz na wengine wengi ingawa hawakuwa waasisi lakini michango yao ni ya kutukuka kama Mshume Kiyate na wengine wengi.

Nilijaaliwa kukutana na Germano Pacha akiwa pamoja na wazee wenzake waliosisi TANU Jimbo la Magharibi wakati wa utafiti wa kitabu cha Sykes.

Germano Pacha anasema kama isingekuwa picha ile waliyopiga siku ile ya kuasisi TANU wangelijitokeza waasisi wengi.

Aliyonihadithia Mzee Pacha na wenzake yanasisimua sana.

Pacha anasema mwaka wa 1953 alitumwa na viongozi wenzake wa TAA Tabora aje Dar es Salaam kuonana na Abdul Sykes kumpa pendekezo la kuunda chama cha siasa.

Pacha anasema aliagizwa kuwa akifika Dar es Salaam aende moja kwa moja nyumbani kwa Abdul Sykes.

Pacha alifanya hivyo na Abdul alimwambia kuwa mipango inafanywa ya kuasisi chama cha siasa.

Pacha alikwenda Pugu kumwona Nyerere na yeye akamweleza kama alivyoelezwa na Abdul.

Hii ilikuwa baada ya ule uchaguzi wa Ukumbi wa Arnautoglo wa 1953 ambao Nyerere alichaguliwa rais na Abdul makamu wake.

Pacha hakupatapo kuandika lakini alinieleza masikitiko yake anaposoma historia ya TANU na kukuta kuwa waasisi wote wale 17 hawakupewa umuhimu wanaostaili.

Pacha alinionyesha nyaraka nyingi za TAA na TANU.

Moja ambayo ilinigusa ni hii, ’’Kumbumbu za Uenezi wa TAA/TANU Western Province.’’

Nilimshauri azipeleke nyaraka zake Nyaraka za Taifa alikataa na kusema maneno mengi kwa uchungu.

Ni wazi kabisa kuwa wazalendo waasisi hawa wa TANU wameondoka duniani wakiwa na kinyongo.

Suali la kujiuliza ni hadi lini tutaendelea kupuuza historia ya wazalendo waasisi hawa 17 wa TANU?

Hivi hata leo Saba Saba siku yao hatuna la kusema kuhusu mchango wao?
 
Ccm yenyewe kwa sasa inaongozwa na genge la wahuni. Nani ataweza kuwakumbuka hao wazeee
 
tatizo baada ya uhuru walisalitiana ndio maana historia yao imefutwa
 
Laki...
Itapendeza ikiwa utatupa habari ya huu usaliti tuboreshe historia yetu.
Kasela Bantu, Bibi Titi Mohamed, Abdul Sykes walipanga hujuma za kumuua Nyerere mpaka wakashtakiwa kwa uhaini na kufungwa jela, ina maana hujui hili? huo ndio usalita wenyewe
 
Kasela Bantu, Bibi Titi Mohamed, Abdul Sykes walipanga hujuma za kumuua Nyerere mpaka wakashtakiwa kwa uhaini na kufungwa jela, ina maana hujui hili? huo ndio usalita wenyewe
Laki...
Kesi ya Kasella Bantu haikuwa ya kumuua Rais.

Kassella Bantu kesi yake ilihusu mauaji yaliyotokea Nzega ya kuuliwa wanaodhaniwa wezi wa ng'ombe baada ya yeye kama Mbunge kuhutubia wananchi wake.

Kesi hii Kasella Bantu alishinda.

Abdul Sykes hakupata katika maisha yake kushitakiwa kwa kosa lolote na alipofariki mwaka wa 1968 Nyerere alihudhuria maziko yake.

Kesi ya Bi. Titi ni maarufu kuwa alishtakiwa kwa uhaini na akafungwa maisha.

Ikiwa mimi nimekosea kwa hayo niliyoeleza hapo juu kwa kuwa sijui nasubiri kusikiliza maelezo yako.
 
Kasela Bantu, Bibi Titi Mohamed, Abdul Sykes walipanga hujuma za kumuua Nyerere mpaka wakashtakiwa kwa uhaini na kufungwa jela, ina maana hujui hili? huo ndio usalita wenyewe
Laki...
Nimekupa jibu kuhusu hayo uliyosema.

Huwa sina kawaida ya kufuatilia mtu niliyempa jibu sawia na yeye
kwa kuona ukweli akawa kimya.

Hapa nimeona nivunje kawaida yangu.

Sasa nakuuliza mbona uko kimya nitafsiri ukimya huu kuwa yale
uliyosema baadhi hayakuwa na ukweli?
 
Mkuu Mohamed Said unaandika mambo muhimu sana kwa taifa. Bahati mbaya ni kuwa historia huandikwa na “washindi”. Kwa hilo, nchi yetu inayofuata utamaduni wa “personality cults”, haijajipambanua. Ni kazi ngumu sana kujaribu kueneza “objectivity” nchini hapa.
 
Mkuu Mohamed Said unaandika mambo muhimu sana kwa taifa. Bahati mbaya ni kuwa historia huandikwa na “washindi”. Kwa hilo, nchi yetu inayofuata utamaduni wa “personality cults”, haijajipambanua. Ni kazi ngumu sana kujaribu kueneza “objectivity” nchini hapa.
Drifter,
Washindi na waandike hatuwezi kuzuia lakini wengine nao wameandika.

Wasomaji sasa wana chaguo.
 
Back
Top Bottom