Wazalendo: Warioba na wajumbe wa bunge jamani muwe makini kwa hili kwa maendeleo yetu

Wazalendo: Warioba na wajumbe wa bunge jamani muwe makini kwa hili kwa maendeleo yetu

mshumbue-soi

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2013
Posts
1,842
Reaction score
1,148
Wanajamvi

Sura ya kwanza ya Rasimu, Sehemu ya Kwanza Ibara 4 (1) inasomeka, "Lugha ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano ni Kiswahili na itatumika katika mawasiliano rasmi ya kitaifa na kiserikali

Wajumbe wa Bunge katiba Taasisi ya Elimu hebu mkaifanyie marekebisho kitumike kufundishia

Kwanini?

-Miaka 50 hakijasaidia sana
-Kiwe rasmi hata katika kufundishia
-TUKI, Udsm ilishaona umuhimu kitumike. Mpaka wana vitabu vya shule za Sekondari tafsiri ya kiswahili

-Ni wakati wa kuachana na kiingereza ambacho kinawafanya wanafunzi wasiweze kwenda zaidi ya walichosoma au kujifunza kwa kuwa lugha sio rafiki.

-Mafanikio ya Elimu yanategemea pia lugha iliyotumika katika kufikia malengo ni wakati kuelewa isiwe tatizo

- Kiingereza kimekuwa KERO kwa Wanaojifunza kuelewa kiwango cha utoshelevu na hata Wanaofundisha.
-Kiingereza wakoloni walitaka tujue walichotaka sio zaidi, "Elimu ya kukaririshwa"

Hivyo isomeke, "....na itatumika RASMI KUFUNDISHIA ELIMU YA MSINGI,SEKONDARI,VYUO na mawasiliano ya kitaifa na kiserikali
 
Ok sio wajumbe watakaoteuliwa toka taasisi ya Elimu bali wajumbe wote wa bunge la katiba mpya ni muda kuwasaidia wasomi wetu katika hili ili Elimu ya miaka 50 ijayo iwe ni kuelewa sio kukaririshwa
 
Back
Top Bottom