Wazalishaji matrekta wachangamkia fursa Tanzania

Wazalishaji matrekta wachangamkia fursa Tanzania

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,712
pindaz_300_182.jpg

KAMPUNI ya URSUS ya kutengeneza matrekta ya kutoka Poland, imeonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania na iko tayari kushirikiana na kampuni ya SUMA JKT kutengeneza matrekta hayo.

Hayo yalisemwa na Rais wa Bodi ya Ursus, Karol Zarajczyk wakati akitoa maelezo ya kampuni yake mwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokutana na wafanyabiashara wenye nia ya kuwekeza Tanzania jana kwenye hoteli ya Sheraton jijini Warsaw, Poland.

Zarajczyk alisema wanataka kujenga kiwanda hicho nchini Tanzania kwa kutambua nafasi ya kijiografia ya mahali nchi ilipo, kuwa ni fursa ya kufungua milango kwa nchi jirani za Afrika Mashariki na Kati.

"Barani Afrika tulianza kupeleka matrekta Ethiopia, Ghana na Guinea. Sasa hivi tumeamua kuja Tanzania na Zambia. Nia yetu siyo kujenga tu kiwanda bali pia kutoa huduma kwa wakulima juu ya uendeshaji na utunzaji wa hayo matrekta," alisema.

Alisema wako tayari kutoa mafunzo kwa vijana wa Tanzania, kama vile chuo fulani ili waweze kuunganisha matrekta hayo hapa nchini na waweze kuyafanyia ukarabati na kutengeneza vipuri vyake pindi ukitokea ulazima wa kufanya hivyo.
"Tunapenda kujenga kiwanda mahali ambapo itakuwa rahisi kupata vijana wa kuajiriwa au vijana wa kutoka chuoni ili iwe rahisi kuwafundisha pia teknolojia tunayoitumia kutengeneza matreka hayo," aliongeza.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu alisema atawasilisha maelezo yao kwa Waziri anayehusika na sekta hiyo ili mawasiliano rasmi yafanyike.

CHANZO: Habari Leo
 
Ingekuwa vizuri kama wana nia ya kujenga kiwanda au viwanda bora serikali ingewaandalia sehemu mikoa mingine mbali na dar ili viwanda viwe mikoani pia
 
Haya mazungumzo badala ya habari kwa miaka tisa sasa tumeshayachoka! Tena yanabore!
 
Ingekuwa vizuri kama wana nia ya kujenga kiwanda au viwanda bora serikali ingewaandalia sehemu mikoa mingine mbali na dar ili viwanda viwe mikoani pia

Fly over zimewashinda, hata barabara ya dampo imewashinda pia, wataweza matrekta!
 
"Kwa upande wake, Waziri Mkuu alisema atawasilisha maelezo yao kwa Waziri anayehusika na sekta hiyo ili mawasiliano rasmi yafanyike."

Sidhani kama Pinda akifika hapa atakuwa bado anakumbuka alichokisema. Akili itakuwa imeishahamia kwenye Katiba Pendekezwa na Umbio za Urais.
 
Back
Top Bottom