Katika mjadala wa muswada wa katiba uliofanyika Zanzibar,wazanzibar waliojitokeza katika mjadala huo sio tu waliupinga muswada huo,bali walisikika wakiukataa na muungano pia.Katika fikra zao wanaamini ya kuwa wao hawanufaiki na muungano kama wanavyonufaika nao watu wa bara.Hekima na busara za kutosha zinahitajika ili kuziondoa kero za muungano.Vinginevyo,muungano upo matatani.
Km wasemavyo makada wa chama tawala, sasa ni wakati wa kufanya maamuzi magumu, lujivua gamba kwa ccm na matakwa ya Katiba mpya kuendane na kuzaliwa kwa tanzania mpya, mawazo ya wengi yasikilizwe, KURA YA MAONI NI MUHIMU KTK KUFANYA MAAMUZI..
Kura ya Maoni?
Tupige kura kuulizwa kama tunataka Uhuru wetu tulioporwa na Tanganyika?
Kwani Mkuu nyinyi mliwahi kuulizwa iwapo mnautaka huu Muungano? Maana sisi hatukuwahi kuulizwa.
Muungano huu hauna uhalali wa kisiasa na kisheria, uvunjike tu.
Baada ya hapo na kama tutakubaliana, tutatafuta njia nyengine ya kushirikiana kwa misingi ya kuheshimiana.
Zanzibar for Zanzibaris.
Hii unayoleta ni kashfa kubwa kwetu waZanzibar.
Kwani siku zote anaedai na kupewa talaka ni mwanamke. Sasa kwa taarifa yako ndani ya muungano hakuna mwanaume wala mwanamke wote ni sawa.
Na hata kama alikuwepo mwanamke basi atakuwa ni Tanganyika kwani baada ya ndoa tu alibadili jina na kujiita Mrs Tanzania. Sisi waZnz tunaitwa wazanzibari kama kawaida hatubadili jina.
Badilisha heading yako