Wazawa hawaheshimiwi kwenye Soka la Tanzania

Wazawa hawaheshimiwi kwenye Soka la Tanzania

prince basho jr

New Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
3
Reaction score
6
MZAMIRU YASINI NI ROHO KWENYE KIWILI WILI CHA SIMBA.

Acha na zile Assist za Clatous Chama acha na ile mikimbio na press za Ntibazonkiza acha na zile Hat trick za Beleke ila pale Simba SC Tanzania yupo mwana Kigoma anaitwa Mzamiru Yassini.

Huyu katika michezo mingi ya Simba ndio amekuwa kiini cha mipango yote ya mchezo uwanjani. Ukimuona chama ana fent ukimuona Ntibazonkiza ana drible mpira basi ujue mpango wa kwanza unaanzia kwa Mzamiru.

Ubora wake kwenye kukaba njia kupokonya mipira na kusogeza pass kwa wakina chama ndio kiini cha ushindi katika kikosi cha Simba.

Mzamiru ile Energy yake pale Lunyasi labda inaweza kukaribiwa na Zimbwe jr ila sio ndani na nje ya Simba kama kuna kiungo wa kariba hii.

Dakika 180 timu ya taifa dakika 90 vs Raja pale Mohammed V kisha dakika 90 Azam complex ni ishara ya ubora na nishati ya kutosha.

Leo tumeona AISHI SALUM MANULA akiomba sub Inonga akitepeta Onyango akipoteza umakini ila Mzamir wa juzi, jana ndio yule wa leo na kesho.

Ila licha ya ubora wote ndani ya kikosi cha Simba sc Mzamir sio kipenzi cha mashabiki wengi wa Simba sc pia sio rahisi kumuona Mzamiru akipostiwa kwenye kurasa za Simba sc ila usishangae kusikia Mzamiru analipwa pesa ndogo kuliko Sawadogo.

May be vijana wetu wa kitanzania wana shida kwenye negotion wakati wa kusaini mikataba ila ifike muda vilabu vyetu navyo vione namna ya kutengeneza chapa za wachezaji wazawa.

Pale England sio tu kuwa wachezaji wa Kingereza wana mawakala bora ila tayari vilabu vya England vimeset standard za Fee na mishahara ya wachezaji wa Kingereza pia wameamua vilabu kutengeneza thamani ya wachezaji wa Kingereza.

Huyu Mzamiru kama ingekuwa sio mzawa angeimbwa na kupostiwa kila mahala ila kwa kuwa ni mzawa hata kwenye social media za Simba sc hana nafasi. Tanzania ni muda sasa wa kuwapa thamani wachezaji wazawa.

A0D56F57-709A-4319-BBEC-EC8B1503797E.jpeg
 
Athuman Idd Chuji
Henry Joseph Sindika
Nizar Khalfan
Haruna Moshi Boban
Amri Kiemba

Sio Mzamiru peke yake walikuwepo hao kwa uchache na hawakupewa thamani yoyote. Ni hulka yetu kutokuthamini vya kwetu
 
Inasikitisha sana angalia hata feitoto dah inauzunisha sana bongo shida sana ndio mana mpole katimka zake

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Punda mechi na Waganda kule Egypt Aucho aliita maji mma.
 
Athuman Idd Chuji
Henry Joseph Sindika
Nizar Khalfan
Haruna Moshi Boban
Amri Kiemba

Sio Mzamiru peke yake walikuwepo hao kwa uchache na hawakupewa thamani yoyote. Ni hulka yetu kutokuthamini vya kwetu
Hii kasumba itabadi ifanyike namna yoyote ile ife, tumekuwq taifa la watu wa ovyoo halafu sisi tunajiona ni wakarimu
 
Back
Top Bottom