WAZAWA: Swala Oil & Gas (Tanzania) Plc will be selling up to 9,600,000 shares at a price of Tanzania


acha unazi wa Mengi, tuko kwenye soko huria, makampuni ya wazawa yanaweza kuwa hata millioni moja, aliyekuambia kampuni lazima iwe moja tu ni nani? tena lazima iendeshwe na mengi? Halafu kama taarifa zangu ziko sawa Mengi mwenyewe tayari ana hisa zake kwenye hii hii swala Oil....:der:
 
Huu ni mtihani mwingine kwa wawekezaji waKitanzania.Ukikumbuka machungu ya TOL,NICOL na Precision Air.Lazima uingiwe na hofu.Ukizingatia pesa hii ni kwa ajili ya utafiti wa Kilosa-Kilombero exploration project,wakikutana na vumbi tupu itakuwa ndio tushazika hizo pesa zetu.
 

Dah,
Kweli aisee!!
 
Hii ya ununuaji hisa inahitaji darasa la kutosha maana kama ingekuwa iko poa wale wenye hela Uswiss wangezileta kuja kununua hisa!
 
Nimeona hayo majina ya wakurugenzi wa hiyo kampuni yumo huyo mtoto wa Mwinyi anayeitwa Abdalla; huyu bwana aliwahi kuja na watu wakaanzisha kampuni ya simu za mkononi ambayo haikufanya vizuri ikabidi ifunge milango hivyo nina wasi wasi na umahili wake!! Hapo tu nimestuka halafu kwenye website yao taarifa nyingine hawazioneshi kwamfano SHAREHOLDER'S COMMUNICATION POLICY haionekani!!!
 
acha majungu wenye fedha zao wache wawekeze hamna kuibiwa kuna sheria za kulinda hisa
 
Kampuni ya Vodacom mlisema wanajinufaisha wachache kwa kuuziana hisa kinyemela ambavyo sio honest sasa wamekuja wa gas na oil mnalalamika ngoja wajuzi wa hii investment ya gas na oil waje wazikwapue zota waanze kula dividend muanze kujutia na kununua principal kwa sharer anayenufaika ni ndoto

Shime tujiendeleze wazawa makampuni mengine hata hutasikia wakikutangazia kwamba kuna hisa zinauzwa sanasana ya kigeni wanapeleka utajiri wote kwao huku tunachwa hola.

Mfano mzuri ni African Barric wameinvest miaka mingi ila awali hisa zao zilikuwa zikisomewa kwenye Stock Exchange huko Canada na London wakati investment iko Tanzania aibu ilioje??
 
wakuu nashukuru sana kwa ushauri wenu. Nilishachukua fomu pale CRDB kwa ajili ya kununua Hisa. Narudi nyuma. Ngoja hela zangu niendelee kuwekeza Viral Angles ambapo faida ni instant.

mkuu naomba maelezo zaidi juu ya viral angels ni nini na jinsi gani ya kuwekeza na vipihiyo faida ya instant inavyopatikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…