Michosho
JF-Expert Member
- Mar 17, 2012
- 662
- 649
Huwa najiuliza; zamani na sasa kuna tofauti kubwa sana katika suala la elimu?? Mbona wengi wetu tulisoma shule za kawaidatulifaulu vizuri? Au kuongea kizungu ukiwa chekechea ndiyo usomi? Au hizo shule za kawaida siku hizi hawafaulu? Mbona wapo wanaofaulu na kuwazidi waliosoma hizo English Medium? Au ni kufuata mkumbo kumpeleka mtoto hizo shule ,au ni fashion wakati uwezo wako ni wa kusuasua? Hivi sasa wazazi wengi wanaamini shule nzuri kwa watoto wao ni English medium schools, wazazi wengi wanapambana kuwapeleka watoto wao katika shule za aina hiyo,na siyo za selikari wakati hali kiuchumi ni ngumu...ugali maharage kila siku.
Karibuni mtoe maoni yenu wakuu
.walau nipate uelewa zaidi kwa hili suala.