Wazazi na english medium: Ni fashion au ni fuata mkumbo?

Michosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Posts
662
Reaction score
649

Utakuta Mzazi yuko nyumba ya kupanga,mtoto yuko English medium ya Tsh million moja(chekechea), kipato cha mzazi ni laki 2.5 kwa mwezi…….., hana kiwanja wala nyumba…..JE, ni sawa?.... kufanya jambo linalozidi uwezo wako eti kisa jirani ako na mtoto aliye English Medium, ni sahihi kweli hii jamani?

Huwa najiuliza; zamani na sasa kuna tofauti kubwa sana katika suala la elimu?? Mbona wengi wetu tulisoma shule za kawaidatulifaulu vizuri? Au kuongea kizungu ukiwa chekechea ndiyo usomi? Au hizo shule za kawaida siku hizi hawafaulu? Mbona wapo wanaofaulu na kuwazidi waliosoma hizo English Medium? Au ni kufuata mkumbo kumpeleka mtoto hizo shule ,au ni fashion wakati uwezo wako ni wa kusuasua? Hivi sasa wazazi wengi wanaamini shule nzuri kwa watoto wao ni English medium schools, wazazi wengi wanapambana kuwapeleka watoto wao katika shule za aina hiyo,na siyo za selikari wakati hali kiuchumi ni ngumu...ugali maharage kila siku.

Karibuni mtoe maoni yenu wakuu…….walau nipate uelewa zaidi kwa hili suala.
 
aaaaaa mdau hilo neno mie muhasibu english medium just a mere house girl/office attendant anayelipwa 60,000 kwa mwezi anamsomesha mtoto nursery english medium term moja laki 3 shule inaterm 4 hayo malipo sasa utacheka
 
Jamani tuache utani,hizi shule za mulugo ni majanga.kijana wangu wa kwanza nilimpeleka hizo.mpaka anamaliza darasa la kwanza hajui kusoma ,kuandika, wala kuhesabu.nikamrudisha la kwanza tena,kidogo anajua kuandika na kuhesabu,kusoma bado.....
 
mkuu, mbona tulijua kusoma na kuandika shule unazoziita za mlugo? kwa nini mwanao kashindwa kusoma katika hzo shule?
 
aaaaaa mdau hilo neno mie muhasibu english medium just a mere house girl/office attendant anayelipwa 60,000 kwa mwezi anamsomesha mtoto nursery english medium term moja laki 3 shule inaterm 4 hayo malipo sasa utacheka

hiyo kali, kufanya jambo lilo nje ya uwezo wako eti nawe ijulikane mwanao yuko English medium, wakati unaumia... bnafsi naona ni noneses..
 
Kwa hali ya maisha inavyokwenda na kwa jinsi serikali isivyokuwa serious kusimamia ubora wa elimu kwa shule zake nakubaliana na wale wanaoamua kuwapeleka watoto english medium. Issue ya kipato ni nyingine. Lakini jiulize; ada ya 1M inalipwa kwa mkupuo? Jibu ni hapana.
Mana yake ni kwamba naweza kujipanga nikalipa hiyo ada taratibu na nikaweza. Mbona wanapotuletea michango ya harusi hawaangalii mishahara yetu?
Mi nashauri kama unahisi mtoto wako atapata elimu bora huko mpeleke na jipange taratibu utaweza.
Muhimu; monitor maendeleo ya mwanao huko alikoenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…