Wazazi wa vijana 5 waliotekwa mwaka 2021 Kariakoo waibuka tena, wamlilia Rais Samia. Wanasema uchunguzi ulikamilika lakini ripoti haijatoka

Wazazi wa vijana 5 waliotekwa mwaka 2021 Kariakoo waibuka tena, wamlilia Rais Samia. Wanasema uchunguzi ulikamilika lakini ripoti haijatoka

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mnakumbuka ile story ya wale vijana watano waliotekwa Desemba 2021 kule Kariakoo.

Hivi karibuni wazazi wa vijana hao wamejitokeza tena kuomba msaada kwani mpaka sasa hakuna kitu kimefanyika ili kujua vijana hao walipo.

================================================

Miaka mitatu ikiwa imepita hadi sasa tangu vijana watano wapotee katika mazingira tata Kariakoo jijini Dar es Salaam, wazazi na ndugu wa vijana hao wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati suala hilo.

Hii ni makala fupi iliyoandaliwa na Global Online TV wakiwahoji wazazi wa vijana hao.

"Mmoja ya wazazi wa vijana hao amesema kuwa kuna kipindi walipata taarifa kutoka kwenye kituo kimoja cha haki za binadamu Tanzania kuwa ripoti nzima ya kutoka kwa vijana hao imekamilika na Jeshi La Polisi wanayo"

Walipojaribu kufuatilia kwa IGP Camillus Wambura kuhusu ripoti na majibu ya wapi walipo vijana hao, waliambiwa waende Central Police, walipoenda waliambiwa mpelelezi wa kesi hiyo ameamishwa na wakapewa mpelelzi mpya ambaye alifungua upya jalada la uchunguzi


 
Walifanya nini hadi kukamatwa?????
Walimtukana JPM nini maana ndo kilikua kipindi chake hicho!!
 
Mungu ibariki Tanganyika mzenji haya hayamuhusu ndio maana kapiga kimya
 
Back
Top Bottom