MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Mimi nikiwa mdau mkubwa wa riadha nimeona niandike huu uzi kupinga comments za kisiasa zinazotolewa na watu mbalimbali kuhusu wanariadha wa Tanzania walioshiriki Olympic Marathon 2024 za Paris.
Comments nyingi ni za kisiasa kutoka kwa watu hata wasiojua utaratibu wa mtu kushirikishi mashindano ya Olympic.
Simbu ni wa pili kushoto
Mwanamichezo kushiriki Olympic kuna vigezo vyake kwa mujibu wa kamati ya Olympic. Tunapoona Tanzania imepeleka wanariadha wawili tu kwenye mashindano sio kwamba nchi haina hela ya kuwapeleka hata wanariadha 1000.
Pia soma: Wanariadha wa 4 kutuwakilisha kwenye mashindano ya Olimpiki huko Paris Ufaransa Mwezi Julai, Kambi kuwekwa Arusha
Ni kwa sababu ya kukosekana wanariadha walikidhi vigezo. Ingekuwa suala ni pesa basi Sultan wa Brunei angejaza watu kwenye Olympic. Lakini kwasababu kuna vigezo vya kiufundi ndo maana tunaona Bahrain, Kazakhstan, USA, Qatar na matajiri wengine wakigawa uraia kwa wakenya, wanajeria na wanariadha wengine wa kiafrika ili kupata washiriki.
Itoshe kusema kwamba kina Simbu na Geay hawakuanza kushiriki mashindano ukubwani. Hao walianzia utotoni ndo maana leo wanawika dunia nzima na ni matajiri. Katika wanamichezo na wasanii wote hapa nchini ni wachache sana wanaoweza kuwazidi pesa hao vijana wawili.
Kuhusu exposure waliyo nayo hata Diamond Platinumz anasubiri. Hao vijana tangu wakiwa teenagers ni kusafiri tu nchi mbalimbali. Majirani zao wa Arusha wanaweza kuwapa ushuhuda.
Ni wito wangu kwa wazazi wenye watoto wenye vipaji kuhakikisha wanawasaidia watoto wao kutimiza ndoto. Pichani ni mwaka 2006 wakati Simbu akiwa kijana mdogo sana. Alishiriki mashindano huko Singida akiwa mdogo sana.
Kwenye hayo mashindano hakufanya vizuri ila kocha aliyeona kipaji chake alimchukua kutoka kwao na kuishi naye Arusha huku akimpeleka shule ya sekondari. Shukrani kwa sponsor wake aliyehakikisha Simbu anahitimu angalau kidato cha nne kwasababu vijana wengi wenye vipaji huwa hata form II hawamalizi.