Binafsi wazazi wangu walikua wakali ila Babà alizidi. Akirudi hujalala saa 3 usiku ni kesi ya jinai. Mchana akirudi kazini saa 9 hujalala ni kosa kubwa sana kwake,kuamka saa 11 jioni
Niwashukuru sana kwa mahitaji ya shule na kila kitu tulipata ila muda wa kukaa na sisi ilikua nadra sanaa.
Badae mama alibadilika akawa anazungumza na mimi kwa baadhi ya mambo.
Nakumbuka nikiwa form six alikua ananipigia simu sana kila weekend.
Kuna siku nilipomaliza form six mama aligundua Nina mahusiano na bint flan hivi mtaani,alinikalisha usiku saa 7 na kuzungumza kuhusu tabia za yule binti ambazo sio nzuri akaniomba niachane nae.
Hii ilinijenga sana,mzee nae akakazia nilichoambiwa na Mama aliponitoa kwenda matembezini na yeye.
Matokeo yalitoka nilifaulu vizuri sana(Hili namshukuru sana Mungu)
nimeona niliseme hili sababu kuna kitu cha kujifunza hapa, nilijifunza wazazi wanalipwa na furaha sana mtoto wao akifaulu,wanasikia faraja kutembea sababu yako.Kuna namna thamani yangu ilipanda mtaani,tulikua kota za kampuni flan hivi morogogo,walimu walionifundisha shule ya msingi waliniomba niwafundishe jioni, wengi walikua wanatafuta credit na kujiendeleza kielimu.Ilinifanya Niongeze viwango vya nidhamu yangu mtaani
Wajomba zangu jitahidini msituamgushe tumiwalipia Ada.
Watoto wangu nazungumza nao sana kwa ukaribu nijue walau changamoto zao za kila siku nikipata nafasi.
Napenda kujua ndoto za wanangu na vipaji vyao nizifanyie kazi mapema ilizimee na kuzaa matunda mazuri kwa Neeema na Baraka za Mungu.