SoC02 Wazazi/Walezi na Jamii sisi ni wajenzi wa tabia za Mtoto

SoC02 Wazazi/Walezi na Jamii sisi ni wajenzi wa tabia za Mtoto

Stories of Change - 2022 Competition

Sister Abigail

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2020
Posts
2,886
Reaction score
9,088
Habari wanajamii,

Nimewiwa kuwaandikia hili.

Tangu zamani kumekuwa na tabia za watoto zisizopendeza,huku lawama akipewa mzazi pekee kwa kigezo cha kushindwa kulea mtoto katika maadili mema. Siku hizi imekuwa kawaida kukuta katika vyombo vya habari vikiripoti mtoto kampiga mwenzie na kumsababishia kifo,ama mtoto wa darasa la tano kamlawiti wa darasa la pili, inasikitisha.

Lakini swali linakuja, huyu mtoto kajifunzia wapi hayo mambo? Kajifunza kutoka kwa nani hayo matendo? Unakutana na mtoto mdogo ila anatukana matusi ya nguoni kayajulia wapi?.

Kiufupi kila siku mtoto amezungukwa na pande mbili,wa kwanza ni Mzazi au Mlezi na wa pili ni Jamii. Pande hizi mbili zina mchango mkubwa katika ujenzi wa Tabia za mtoto. Mlezi wa kwanza wa mtoto ni mzazi, na mlezi wa pili ni jamii. Ikiwa mzazi atafanya vema katika malezi, basi jamii ikishindwa bado kuna uwezekano wa mtoto kuharibika. Malezi tunayowapa ndio yanayojenga tabia zao. Sisi ni mfano wa wao waenende vipi, wanajifunza kutoka kwetu Matendo yetu na mienendo yetu

Kisaikolojia mtoto anafuata zaidi matendo kuliko maneno. Matendo yanaongea kwa sauti kuliko maneno. Utakachokifanya ama kutenda ndicho atakachokopi kwako na kitakuwa tabia yake.

Mfano mzazi unavaa mavazi yasiyo ya staha,nusu utupu kisha unatoka mbele zake, mwanao akiamua kuvaa mavazi ya aina hiyo unamfokea avae kwa kujistiri. Mwanao amechagua mavazi kama hayo sababu anaiga kutoka kwako, wewe wewe ni mwalimu wake aenende vipi. Kama mwalimu umefanya hivo yeye mwanafunzi anaona sawa pia. Mzazi unatoa lugha chafu za matusi mbele ya mwanao, kisha yeye akitukana unamkemea kwanini?kama wewe mtu wa mfano unatukana kwanini yeye asitukane? Kama yeye anakosea wewe je hukosei?

Wewe ndie mtu wa mfano kwake, utakachokifanya ndicho atakachokifanya. Mama kuwa mwanamke ambae unataka binti yako aje kuwa. Baba kuwa mwanaume ambaye unataka kijana wako aje kuwa.

Mifano halisi wa kizazi kilichoharibika kutokana na malezi mabovu kutoka kwa jamii na wazazi ni kundi la kihalifu maarufu kwa jina la Panya road. Hili ni genge la kufanya uhalifu lenye watoto kuanzia miaka 12 kuendelea. Limekuwa likipora na kujeruhi maeneo mbalimbali kwa miaka mingi. Hawa ni mfano na matokeo ya malezi mabovu kutoka kwa jamii na wazazi ama walezi.

Hili ndicho kizazi kilicholelewa kikiwa kimezungukwa na jamii yenye mambo ya hovyo,mazingira yao ukipita vichochoroni utakuta wamekaa na wavuta mihadarati, watumiaji wa madawa ya kulevya. Ukahaba upo hadharani. Kumekithiri matamasha yasiyo na maadili, muziki usio na maadili, ukabaji na wizi. Jamii ndio hii mzazi hapo ana kazi kubwa hata afanyeje bado mlezi wa pili ambae ni jamii atamuharibia mtoto tu.P ande mbili zote zina majukumu zinategemeana matokeo leo tunayaona wamekuwa wahalifu sugu.

Ukija kwa upande wa mzazi anaweza pia yeye ndo akawa chanzo cha uharibifu wa gabia za mtoto. Mtoto anaishi katika familia iliyojaa unyanyasaji wa kijinsia, vipigo, ulevi na matusi na ubakaji ikiwa atashuhudia haya matendo na tabia ikawa endelevu anaweza kuyachukulia kitu cha kawaida, saikolojia yake itakubali hayaonayo toka kwa mzazi au mlezi na hivyo ndio matokeo zitakuwa tabia zake za kesho.

Tunachokifanya leo kama jamii au wazazi ndio kitaamua tuwe na vijana wa aina gani hapo kesho

MAONI YANGU
Tunaweza kujenga kizazi chenye maadili mema kwa sisi kubadilika na kuwa mfano mwema wa kuigwa kitabia na kimatendo mbele ya watoto kwa faida yao na yetu pia.

Mzazi au mlezi unaweza mlea mwanao katika misingi inayofaa na kuwa mfano mwema kwake, lakini ikiwa jamii inakuharibia tafadhali chukua hatua watoto wanajifunza kupitia watu wazima kwa hali hiyo wanahitaji mazingira salama ambayo hayatawaathiri kisaikolojia, kimatendo na kimaadili.

Kwa upande wa jamii pia tuna wajibu katika malezi ya watoto kuwalinda dhidi ya mazingira yasiyofaa, kuwaepusha na mazingira yenye vitendo hatarishi hata kama sio mtoto wako wa kumzaa kuna msemo usemao "mtoto wa mwenzio ni wako"

Matokeo ya kesho yanaweza kukuathiri ama kukufaidia kutokana na mtoto alikopitia hata kama sio wako wa kumzaa ama kumlea

Mfano halisi ni panya road, Leo wametoka kwenye jamii fulani ila wamekuwa athari mbaya kwa jamii tofauti.

Tuna wajibu na tuna jukumu La kuwalinda watoto ,kwa manufaa yetu na kizazi kijacho.

Ni Mimi
Abigail.
 
Upvote 1
Wazazi wajitahidi kukaa na watoto wao kwa ukaribu sana kwa malezi Bora ndani ya pikindi cha miaka 4 hadi 13. Tofauti na hapo kumbadilisha mtoto kwenye Tabia fulani ni ngumu tena...........
 
Pamoja na yote wazazi wajitahidi kukanawatotowao kwaukaribu sana kwamalezi Bora ndani ya pikindi cha miaka 4 hadi 13. Tofauti na hapo kumbadilisha mtoto kwenye Tabia flani ni ngumu tena...........
Ni sawa lakini ikiwa mzazi atakuwa karibu na mtoto itasaidia dhidi ya jamii?
Wewe huku unamjenga,yeye Kule anambomoa
 
Back
Top Bottom