SoC02 Wazazi/walezi ni suluhisho, ufaulu mdogo somo la Hisabati

Stories of Change - 2022 Competition

MSOPE MSOPILE

New Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
3
Reaction score
1
Hisabati ni somo linalohusisha namba, maumbo, mafumbo, uhusiano baina yao pamoja na vipimo mbalimbali (merrium webster). Sehemu kubwa ya somo hili ni namba 0 mpaka 9 ambazo humtaka mwanafunzi kuhudhurisha ubongo na fikra katika kutegua changamoto mbalimbali. Takwimu zinaonesha kumekuwa na ufaulu mdogo sana katika somo hili kuanzia msingi, sekondari, na vyuoni.

Ufaulu wa somo la hisabati kidato cha nne katika miaka mitano iliyopita​

2020​
20.12%​
2019​
20.03%​
2018​
20.02%​
2017​
19.19%​
2016​
18.02%​
chanzo : Baraza la mitihani la taifa (Necta)

Tafsiri fupi ya jedwali hili katika kila wanafunzi 100 waliofaulu ni 20, hii ni tofauti ukilinganisha na masomo mengine mfano kiswahili ufaulu ni 84% ikimaanisha katika kila wanafunzi 100 waliofaulu ni 84 (chanzo: necta.go.tz) .

Kwanini wanafunzi wengi wanafeli somo la hisabati ?

Baadhi ya changamoto zinazopelekea hisabati kuwa mzigo kwa wanafunzi wengi kitaifa na hata kimataifa nikama zifuatazo :
  • Mtazamo hasi juu ya somo hili, jamii zetu zinaamini hesabu ni ngumu na haziwezekani labda uwe umerithi kwenye familia yenu yani nikipaji maalum, uelewa ambao sio uhalisia kwani hisabati ni somo zuri na lenye faida nyingi sana ukilijua na ukijituma.
  • Uwiano mdogo baina ya walimu na wanafunzi, idadi ndogo ya walimu kwenye somo hili husababisha walimu kushindwa kutimiza majukumu yao kwa ufanisi zaidi mfano SHULE YA SEKONDARI YA IFWAGI wilaya ya MUFINDI iliyopo mkoa wa IRINGA yenye wastani wa wanafunzi 600 ina walimu wawili tu, hii huleta ugumu kwa walimu kutimiza majukum yao.
  • Uhaba wa vitendea kazi, kumekuwa na upungufu wa vitendea kazi kama vitabu vyakufundishia, hii hupunguza kasi ya wanafunzi kufanya mazoezi na hisabati inahitaji mazoezi mengi, wito wangu kwa wazazi wengi wanauwezo wa kununua vitabu hivi japo kimoja ila wanapuuzia kwani ni wastani wa shilingi 12,000/= tu .
  • Mbinu duni zakufundishia, walimu wengi wamekuwa wakibakia kwenye matumizi ya ubao na chaki katika kufundisha somo hili hivyo wanafunzi wengi hushindwa kuhusisha uhusiano wa somo hili na mazingira wanayoishi. Walimu wajitahidi kubuni zana mbalimbali za kufundishia ili kuleta uhalisia kwenye somo hili. mfano hesabu za maumbo, walimu wajaribu kuchonga maumbo halisi ili kusaidia uelewa wa wanafunzi, wengi hawajui kimo, urefu na upana ni upi n.k

Mbinu (suluhisho) ufaulu mdogo somo la Hisabati

Mbinu hizi zinaangazia wazazi/walezi namna ya kuwajenga wanafunzi kuanzia shule za awali na msingi kujua na kupenda hesabu ili kuongeza ufaulu
  1. Mahusiano bora baina ya mzazi/mlezi na mtoto, wazazi/walezi wanayo nafasi kubwa kuwezesha watoto wao kujua hisabati katika makuzi yao kabla hata yakufika shule, mzazi anatakiwa kumfanya mtoto aone hisabati ni somo linalowezekana pale juhudi inapofanyika na sio kuwa wakwanza kumtisha mtoto na kumpa hofu, wazazi/ walezi watumie fursa mbalimbali kuwafanya watoto wapende hisabati mfano mwambie akuhesabie matunda wakati mkiwa mezani au jikoni, mfundishe hesabu za mbalimbali kama vile nusu (1/2), robo (1/4) kwa uhalisia kwakukata tunda kama apple vipande viwili sawa au vinne, ajue vipimo hata vya urefu wake au urefu wa chumba chake, au kama tayari ana mdogo wake unaweza mpa futi ampime hii itamjengea kujiamini. chanzo : www.phycopost.org
  2. Orodha ya kuzidisha (12x12)/ Mathematical table,wanafunzi wengi huanza kuchukia hisabati pale wanapokupambana na hesabu za kuzidisha na kugawanya, hasa wanafunzi wadogo wa msingi huu ndio umri muafaka anapoingia darasa la tatu hadi la nne mwezi wa sita awe amejua orodha hii bila kusitasita, Ni jambo gumu sana kwa mwalimu mwenye wanafunzi zaidi ya mia moja kumsimamia kila mwanafunzi hivyo wazazi/walezi tumia mbinu zifauatazo a) kama uko bize kumsimamia mwenyewe ajue hii orodha, mtafutie mwalimu lengo ni moja tu sio kuburuza mada zote ni orodha hii tu ahakikishe ameijua sio jambo gumu b) fuatilia maendeleo yake pale unaporudi kutoka kwenye shughuli zako kwa kuchukua hii orodha na kumuuliza baadhi ya maswali akipata mpongeze akishindwa mpe adhabu ndogo ndogo ili aweke juhudi na ataweza bila shaka
  3. Kuelekea darasa la tano, Hapa hakikisha mwanafunzi huyu anajua mada zifuatazo maana mara nyingi wazazi au walezi wanawapeleka shule binafsi au masomo ya ziada bila kupata matarajio chanya, hii ni husababishwa na baadhi ya walimu kuchukua tu fedha au kuzidiwa na majukum hivyo hizi ni mada muhimu kwa mwanafunzi azijue hizi a)Hasi na chanya (intergers) b) sehemu (fractions) c) desimali ( decimals) d) asilimia (percentage) hizi zitamsaidia na kumjenga kwanza kulipenda hili somo atajiona ni mwepesi na hatakuwa na hofu kwenye mada kama maumbo, na nyenginezo za sekondari na hata chuo.
  4. Mazoezi, hisabati ni somo linalohiataji mazoezi mengi hivyo wazazi/walezi ni wajibu kuhakikisha mwanafunzi anafanya mazoezi mengi na mara kwa mara pamoja na kushiriki katika majaribio ya kila wiki katika shule yake au shule jirani ili kumpa ufanisi zaidi.
  5. Your browser is not able to display this video.

Faida za somo la hisabati

Wanafuanzi wengi kwakutojua faida za somo hili wamekuwa wakipata wastani wachini mno na hata wengine kukosa alama moja, zifuatazo ni baadhi ya faida za somo la hisabati
  1. Mantiki (reasoning), hesabu zinachangamsha ubongo na fikra, Ugunduzi uliofanywa na Dr. Tanya Evans wa stanford university ulionesha wanafunzi wanaofanya hesabu mara kwa mara wana uwezo mkubwa wakimantiki kuliko ambao hawafanyi hesabu.​
  2. Msingi wa masomo mengine, mwanafunzi anaefaulu hisabati anakuwa na uwezo mkubwa wakufaulu masomo mengine yote yaliyobaki.
  3. Mipango yakifedha na uchumi, hesabu husaidia kupanga bajeti mbalimbali na uchumi kuanzia ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla .
  4. Fani/Kazi, Kuna kazi nyingi ambazo ili uweze kufikia na kuhitimu kigezo kimoja wapo ni kufaulu vizuri somo la hisabati mfano ukandarasi, udaktari, ualimu, uanasheria, uhasibu, afisa ugavi, wana uchumi n.k​
  5. Hutumika viwandani, kwenye viwanda vya soda, sabuni, na vipimo vya Afya n.k​

hitimisho

Nipende kuipongeza serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuipa elimu kipaumbele na kuifanya bure. Wazazi/walezi wengi kwakupenda elimu bora wamejaribu kuwapeleka watoto wao kwenye shule binafsi ambazo zinamchango mkubwa kwa juhudi zao ila somo hili bado limekuwa pasua kichwa hasa kidato cha nne.

Mara nyingi lawama hizi hupewa wanafunzi, shule, walimu, au serikali husika bila kuangalia upande wa wazazi au walezi mchango wao katika kupunguza au kuondoa changamoto hii. makala yangu hii imegusia namna gani wazazi/walezi wanahusika kutatua changamoto ya somo la hisabati.

marejeleo

www.necta.go.tz
www.tie.go.tz
https://scholar.google.com-Tanya evans
https://www.bbc.com-matokeo somo la hisabati kisado cha nne
 
Reactions: K11
Upvote 0
Nimeona na kusoma vyema!! Hiii kitu Kila mmoja wetu aisome kama ana mtoto
 
Hongera kwa kazi nzuri.
Binafsi uliyoyaongea yana aksi uhalisia ktk somo la hisabati.

Wazazi wengi wana hulka ya kuilaumu serikali na walimu huku wao wenyewe wakijitenga mbali juu ya kusaidia wanao majumbani mwao.

Nimesoma hisabati mpaka ngazi flani kwa mafanikio kwa sababu mzazi wangu alinijengea mazingira rafiki ya kulifaulu somo hilo tangu nikiwa shule ya msingi.
Kila siku usiku ilikuwa lazima tufanye maswali kadhaa ya hisabati ndipo ulale, nilijikuta ninapenda somo hilo hatimae nikamaliza darasa la saba nikiwa na msingi mzuri ulioniwezesha kulimudu somo hilo hadi ngazi ya juu.


Mafanikio ya mwanao yanaanza na wewe mzazi/mlezi.
 
Umeandika vema. Ila kuna jambo moja umelisahau nalo ni msingi mbovu wa mwalimu/walimu anaefundisha izo hesabu. kama ulivosema hesabu ni somo linalohitaji reasoning, mwanafunzi anatakiwa aweze kuhusianisha kati ya yale anayosoma na maisha yake ya kawaida. sasa hapa unakuta mwalimu naye elimu yake ni ungaunga mwana nayeye unakuta mweupe kichwani hana hizo mbinu za kufundisha au nayeye kapangiwa tu afundishe hilo lakini hajui hajui vizuri hizo hesabu zenyewe, matokeo yake mwalimu anaishia kuwapacha tu madogo na hapo ndo unakuta ndo unakuwa mwisho wa madogo kulipenda hill somo wataanza kumchukia huyo mwalimu na somo lake mazima. kifupi hawa walimu na wao ilibidi wawe wanapewa mtihani kutest uwezo wao kwenye masomo wanayofundisha kuna ndoto nyingi sana za madogo zinakufa kwa sababu hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…