Wazazi wenye hasira kali wamevamia Shule iliyopo Meru na kuchinja ng’ombe

Wazazi wenye hasira kali wamevamia Shule iliyopo Meru na kuchinja ng’ombe

Rahma Salum

Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
30
Reaction score
59
Imetokea tafurani katika shule ya msingi Mbajone iliyopo kaunti ya Meru nchini Kenya baada ya wazazi kuvamia shule hiyo na kushinja ng’ombe dume wawili kwa madai ya kuwa shule ilitaka kuwauza bila kufuata utaratibu maalumu.

Wakiwa wamebeba majani huku wakiimba nyimbo takribani wazazi 90 wameshindwa kuzuiliwa na polisi pamoja na chifu wa eneo hilo na kuvamia eneo la shule wakidai kufanyiwa dhuluma na shule hiyo.

Wazazi hao wamechinja ng’ombe wawili na kugawana kilo 254 za nyama na zingine kuuza kwa Shilingi laki mbili ya Tanzania.

Julius Mwirigi mmoja wa wazazi katika shule hiyo amesema, wanalipa kiasi cha Sh. 1,500 za Kenya katika Jumuiya ya Wazazi na Walimu kwa ajili ya mahitaji mbalimbali lakini uongozi unauza vyakula na mifugo. Ameongeza kuwa ng’ombe walinunuliwa kwa ajili ya kuchotea maji ili kupunguza gharama lakini bado shule imekuwa ikiwadai wazazi pesa ya gharama za maji.

Wazazi wanadai kuwa mifugo mbalimbali kama Nguruwe, na mifuko ya mahindi inayomilikiwa na shule imekua ikiuzwa bila kufuata utaratibu wa halali. Vilevile wamedai kuwa wamekuwa wakiambiwa na shule kupanda mazao mbalimbali ila hawajawahi kunufaika na mazao hayo.

Mzazi mmoja amesema kuwa wanaandamana kupinga ukosefu wa uwazi unaotendeka shuleni hapo.

Akizungumza kupitia simu Katibu Mkuu wa KNUT wa Meru Caxton Miungi ametetea uongozi wa shule kwa kusema maindi yaliuzwa kwa ajili ya kulipa deni la madawati ya shule. Amesema wazazi hawajachangia kiasi chochote kwa ajili vifaa vya shule baada ya shule kufungwa mwezi machi.

“Nadhani kulikuwa na uchochezi kwa vile baadhi ya watu walishindwa kupata zabuni. Walikuwa wamekwenda hapo awali na kuvuna vyakula”. Amesema Miungi.

Chanzo: Angry parents storm Meru school, slaughter bulls
 
Nandee, tutiagitwa ni mparaa kaere hendimasta! [emoji1] Wameru hawapendagi ujinga.
 
Back
Top Bottom